• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri wa Afya Awataka Waganga Wakuu Kusimamia Matumizi ya Magari ya Kubebea Wagonjwa

Posted on: July 13th, 2018

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance ) kubeba watu au kitu chochote tofauti na wagonjwa na akawaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini,  kusimamia matumizi ya magari hayo na kuhakikisha yanatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kwa mujibu wa mwongozo.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo Julai 12, 2018 katika uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuunganisha jamii hasa zile zilizo mbali na vituo vya tiba, ambao umezinduliwa katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa na mfumo wa Huduma za Afya ambao umelenga kupunguza vifo vya mama na Mtoto mkoani SIMIYU.

“Nimesikitishwa sana na kitendo cha gari la kubebea wagonjwa la Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kubeba dawa za kulevya, ninakemea jambo hili kwa nguvu zangu zote na ninawataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kusimamia matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa “ alisema Waziri Ummy Mwalimu

“ Ni marufuku gari la kubebea wagonjwa kubeba kitu tofauti na mgonjwa, yeyote ambaye tumemkabidhi gari la kubebea wagonjwa tutamchukulia hatua kali pale ambapo atakiuka mwongozo wa matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa, nalipongeza sana jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua na ninamtaka Mkurugenzi wa Halmashauri husika kuwasimamisha kazi mara moja dereva na wote waliohusika na gari hilo kubeba mirungi” alisisitiza.

Akizundua mradi wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Waziri Ummy amewashukuru wafadhili wa mradi huu Amref Health Africa Tanzania chini ya Ufadhili wa Serikali ya Ireland kupitia Shirika la Irish aid  ambao utatekelezwa kwa kushirikiana na Benjamin Mkapa Foundation na Halmashauri za Itilima na Misungwi(Mwanza) ukiwa na lengo la kupunguza vifo vya mama na Mtoto.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaajiri  Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoka katika Halmashauri au wilaya husika na si vinginevyo.

Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga ameomba Zahanati ya Lagangabili ipandishe hadhi kuwa kituo cha afya kusogeza huduma kwa wananchi, jambo ambalo limefafanuliwa na Mhe.Waziri kuwa zahanati hiyo haitapandishwa hadhi mpaka itakapojengewa miundombinu muhimu na akaahidi kutafuta shilingi milioni 400 kwa kushirikiana na wadau, ili kuwezesha ujenzi wa wodi ya wazazi, mama na mtoto na jengo la upasuaji.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema viongozi wa Mkoa wa Simiyu wanaunga mkono juhudi za Serikali na wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya Afya nchini, na kumhakikishia Waziri Ummy kuwa fedha yoyote itakayotolewa katika Mkoa huo itasimamiwa ipasavyo na kuleta matokeo chanya.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Amref Dkt Aisa Muya amesema mradi huo utasaidia kuunganisha  wananchi walio mbali na vituo vya tiba kupunguza vifo vya mama na mtoto chini ya miaka mitano, kutoa huduma za awali kwa jamii, kutoa elimu kuhusu njia bora za kuepukana na magonjwa, kutoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia na kukusanya takwimu mbalimbali za afya ya jamii vijijini.

Akizungumza kwa niaba ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii Nkwimba Edward amesema wahudumu hao wako tayari kuhudumia jamii kwa kutoa elimu kuhusu mambo mbalimbali ya afya na akaomba Serikali na wadau waone namna ya kuwawezesha kupata usafiri wa kuwafikia wananchi.

Mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha miaka miwili katika  Wilaya mbili ambazo ni Wilaya ya Itilima inayotarajia kuwa na wahudumu wa afya ngazi ya jamii 102 na Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza itakayokuwa na wahudumu wa afya ngazi ya jamii 113.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU UZINDUZI WA MRADI HUU:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/07/waziri-wa-afya-awataka-waganga-wakuu_13.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa