• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Mkuchika Aagiza Halmashauri Kutenga Maeneo ya Kuanzisha Vituo vya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara

Posted on: July 27th, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya uanzishwaji vituo vya urasimishaji biashara kwa wananchi ili waweze kuondokana na umasikini.

Agizo hilo limetolewa na kwa naiba yake na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga katika uzinduzi wa kituo kimoja cha urasimishaji na uendelezaji biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Amesema MKURABITA ndio nyenzo muhimu ya kuwawezesha, kuibua na kuendeleza uwezo wa wananchi kuwa wawekezaji wa ndani wanaowajibika kutengeneza mtaji, soko, ajira na kujenga uchumi wa viwanda ndani ya mfumo rasmi, hivyo ipo haja kwa halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya vituo vya urasimishaji biashara  ili kuwasaidia wananchi.

“ Ni matumaini yangu kuwa vituo vya kurasimisha biashara vitatumika pia kutambua na kuzitumia fursa za uwekezaji ambazo zinatengenezwa na kuimarishwa, nitumie fursa hii kuzitaka Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa vituo hivi katika kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda vinavyomilikiwa na wananchi” alisema Kiswaga akisoma hotuba ya Waziri Mkuchika .

Aidha, amewahamasisha wafanyabiashara na wananchi wote mkoani Simiyu kutumia huduma zipatikanazo katika vituo vya kusajili na kuendeleza biashara zao, huku akiwasisitiza wafanyabiashara wadogo kama mamalishe, wamachinga na waendesha bodaboda kutumia Kituo cha Bariadi, ili waweze kujiondoa katika mfumo usio rasmi na kuingia katika mfumo rasmi wa uchumi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Daniel Ole Njoolay ameiomba Serikali kutoa nyenzo za kutosha za kusukuma urasimishaji na uendelezaji wa biashara kukuza mitaji ya wafanyabiashara kwa kuwa hadi sasa utafiti unaonesha kuwa kuwa zaidi ya asilimia 90 ya biashara si rasmi.

Mwenyekiti Mstaafu wa mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) John Chiligati ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu hususani Bariadi kutumia hati miliki za kimila kama dhamana ya kupata mikopo ya kuendeleza kilimo, kuanzisha viwanda na biashara.

Mtendaji mkuu wa MKURABITA Seraphia Mgembe amewashukuru wote waliopata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara na kuahidi kuwafuatilia na kuhakikisha kuwa miaka ijayo waweze kufanikiwa kiuchumi.

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara wameishukuru Serikali kwa mpango huo kuanzisha mradi wa kituo kimoja cha urasimishaji na uendelezaji biashara, kupitia MKURABITA na kuomba waendelee kupewa mafunzo ili wawze kunufaika na biashara zao.

“Tunaomba tuendelee kupigwa msasa zaidi na zaidi ili tuweze kutunza mahesabu ya biashara zetu vizuri, tuweze kulipa kodi na kuendeleza biashara zetu katika mfumo ulio rasmi” alisema Mashaka Than mfanyabiashara kutoka Bariadi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichofunguliwa Julai 26, 2018 kitatoa huduma za leseni za biashara, usajili wa biashara, huduma za kibenki, TRA, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, wakala wa vipimo na huduma za kampuni binafsi ya GODTEC.

MWISHO

KUPATA HABARI PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuchika-aagiza-halmashauri.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa