• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Lukuvi awataka Wakazi wa Lamadi, Busega kurasimisha Makazi yao

Posted on: April 28th, 2017

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) amewataka wakazi wa Lamadi wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, kurasimisha makazi yao katika kipindi hiki ambacho zoezi la urasimishaji makazi kwa gharama nafuu linaloendelea wilayani humo.

Waziri Lukuvi ametoa wito huo leo wakati wa zoezi la kuhamasisha urasimishaji makazi yalioendelezwa kiholela  na kukabidhi  hati miliki 122  kwa wananchi wenye maeneo yaliyorasimishwa katika Kijiji cha Lamadi.

Lukuvi amesema Lamadi ni Mji wa Kibiashara  hivyo wakazi wake wanapaswa kujenga nyumba zao katika maeneo yaliyopimwa na kutolewa hati ili waishi katika makazi rasmi na salama.

“Mhe.Rais mpendwa wenu ametuagiza kuja Lamadi kurasimisha makazi yaliyokuwa holela ili yawe makazi salama na rasmi, huu ni upendeleo maalum ametoa kwamba waliojenga katika maeneo haya yanayoitwa makazi holela wengi ni maskini na siyo makosa yao, inawezekana wakati wanajenga hakukukwa na viwanja vilivyopangwa na kupimwa na Serikali” alisema

“Mhe.Rais ameagiza watu wote wanaotaka kushiriki zoezi hili wachangamkie fursa hii, ametoa ofa kuwa ninyi ambao mlijenga siku nyingi na mnataka kuongeza thamani ya nyumba zenu mtoke kwenye mtaji mfu na kufanya majengo yenu yatumike kama mtaji wa maendeleo” alisisitiza.

Lukuvi amesema wananchi watakaporasimisha maeneo yao watapata fursa ya kutumia hati miliki zao kupata dhamana ya mikopo katika benki mbalimbali kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.

Aidha, amesema ofa hii ya kurasimisha maeneo ni ya muda tu,  hivyo akawataka wakazi zaidi ya 5000 waliopimiwa viwanja vyao kulipia kabla ya tarehe 30 Juni 2017 ili waweze kupewa hati miliki za maeneo yao na ambao bado hawajapimiwa waone umuhimu wa kupima na kulipia viwanja vyao pia kabla ya muda huo.

Amesema  wananchi wanapaswa kusaidiana na Uongozi wa Wilaya ya Busega  katika kufanikisha zoezi la urasimishaji kwa kuchangia gharama kidogo ili wapimiwe, warasimishiwe, wawekewe alama za mipaka, wapewe ramani na kupewa hatimiliki za maeneo yao na akawataka pia kurasimisha maeneo ya mashamba  na kuyatafutia hati.

Wakati huo huo Mhe.Lukuvi amewataka wananchi wote waliopata hati na wale watakaendelea kupewa kulipa kodi ya ardhi ya kila mwaka kwa Serikali na wale watakaokaidi kulipa kodi hiyo hati zao zitafutwa.

Akizungumza baada ya kupokea hati kutoka kwa Waziri Lukuvi, Mzee Musa Metusela Kole mkazi wa Lamadi, ameishukuru Serikali kwa kurasimisha maeneo yao kwa gharama nafuu na huduma nzuri kutoka kwa wataalam ambao waliwafuata wananchi katika maeneo yao na akatoa wito kwa wananchi wengine kurasimisha maeneo yao ya makazi na mashamba pia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Anderson Njiginya amesema zoezi la urasimishaji ardhi kwa wakazi wa Lamadi limechangia kuongeza mapato yatokanayo na ardhi kwa Serikali, kupunguza migogoro ya ardhi baada ya kupima na kuweka mipaka ya kudumu katika viwanja na kuwawezesha wananchi kutumia hati za maeneo yao kwa shughuli zao za kiuchumi.

Zoezi la urasimishaji wa makazi katika Kituo cha Kibiashara Lamadi lilianza Mwezi Julai 2016 hadi sasa ambapo shughuli ya utambuzi wa miliki umekamilika kwa kupata viwanja 5223  na shughuli ya umilikishaji Viwanja ilianza Aprili 11, 2017 ambapo hadi sasa hati 138 zimeandaliwa kati ya hizo 122 zimekabidhiwa leo kwa wamiliki na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb).

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa