• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Kairuki aagiza SUMA JKT Kukamilisha Ujenzi Kituo cha Umahiri Simiyu Januari 2019

Posted on: November 23rd, 2018

Waziri wa Madini Angela Kairuki amemwaagiza Mkandarasi anayejenga Kituo cha umahiri cha Madini mkoani SIMIYU, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kukamilisha ujenzi ifikapo Januari 2019, ili kiweze kuwasaidia wachimbaji Katika masuala mbalimbali ikiwa ni kupata mafunzo ya uchimbaji wenye tija.

Kairuki ametoa agizo hilo alipotembelea na kuona hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Kituo hicho unaoendelea katika eneo la Nyaumata makao makuu ya mkoa wa SIMIYU Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.

Kairuki amesisitiza usimamizi uimarishwe zaidi na fedha ziweze kutolewa kwa wakati ili jengo hilo liishe katika muda uliopangwa, huku akiupongeza uongozi wa mkoa wa SIMIYU kwa kukubali kutenga eneo la ujenzi wa kituo hicho.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amesema Wizara ya madini itahakikisha inawasadia wachimbaji wa chumvi mkoani Simiyu ili chumvi inayozalishwa iweze kuwa bora na yenye uwezo wa  kushindana katika soko, huku akiwakumbusha wenye leseni za Madini kuzitumia.

“ Kama Wizara tutashirikina na mkoa wa Simiyu katika kuhakikisha wachimbaji wanachimba kwa tija lakini pia kuleta migodi ya mifano na namna za nyingine  ya uchenjuaji, pia  ikiwemo na hiyo chumvi, ambayo tutahitaji izalishwe  katika ubora, ushindani na kuwekwa katika vifungashio bora”

“Tuendelee kuhamasisha wachimbaji wengi zaidi kuendelea kuchimba wasishikilie tu leseni,tunataka kuona ule msamaha uliotolewa na Mhe. Rais kutoka tozo 16 hadi kufikia tozo 09 kwenye chumvi uwe na faida kwao” alisema Waziri Kairuki.

.

Kwa upande wake Mkurugenzi mwendeshaji kutoka SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyonyi amesema watatekeleza maelekezo ya Mhe.Waziri na kubainisha kuwa hadi sasa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 35, kufikia Januari 22, 2019 litakuwa limekamilika na mpaka kukamilika kwa litagharimu takribani shilingi bilioni 1.3.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka uwepo wa kituo cha Umahiri Mkoani hapa utasaidia kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wakubwa wa chumvi katika Wilaya ya Meatu, pamoja na wazalishaji wengine kwa ujumla ambao watajikita katika utengenezaji wa chumvi hali itakayosaidia wananchi Simiyu na maeneo mengine nchini kutumia chumvi itakayozalishwa Meatu badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

Ameongeza kuwa upembuzi yakinifu juu ya uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza chumvi wilayani Meatu umeshafanyiwa upembuzi yakinifu na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kijamii na Kiuchumi (ESRF) na unatarajiwa kuwa mradi mwingine mkubwa wa Wilaya hiyo baada ya mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa.

Aidha, amesema kukamilika kwa kituo hicho kutachangia kutoa mwanya na fursa kwa wananchi wa Simiyu kuwa na uwekezaji mwingine(madini) zaidi ya kilimo na mifugo, huku akibainisha kuwa kitachangia pia kukaribisha wawekezaji wengi kutokana na kuwepo kwa uhakika wa mahali pa kupata mafunzo na kupima sampuli mbalimba za madini .

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:- 


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa