• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wauguzi Waomba Ada ya Leseni za Uuguzi zipunguzwe

Posted on: October 1st, 2019

Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wameomba Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini(TNMC) kupunguza  gharama za ada ya leseni za uuguzi ambazo wamedai kuwa ni kubwa na zinaathiri vipato vyao.

Ombi hilo limetolewa na Katibu wa Chama cha wauguzi Tanzania Bara(TANNA) Bw. Sebastian Luziga wakati akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipofungua Kongamano la kisayansi na Mkutano wa 47 wa wauguzi kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Oktoba 01, 2019 Mjini Bariadi.

Luziga amesema awali ada hiyo kwa ngazi ya astashahada ilikuwa 20,000/=  stashahada na shahada na shahada ya uzamili  ilikuwa shilingi 40,000/=, hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la ada ambapo astashahada wanapaswa kulipa shilingi 40,000/=, stashada 60,000/=shahada 80,000 na shahada ya uzamili na uzamivu ni 120,000/=.

“Ongezeko hili ni kubwa na linaathiri sana kipato cha wauguzi  kwani hakuna uwiano kati ya kupanda huko kwa ada na ongezeko la mshahara; kupitia Wizara ya Afya tunaomba lishughulikiwe upya kwa kufuata utaratibu wa kushirikisha wadau,” alisema Luziga

Akizungumza mara baada ya kupokea risala hiyo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameahidi kulifikisha suala hilo pamoja na mengine yaliyowasilishwa kwa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, huku akiwaomba viongozi kulitafakari kwa upya ongezeko la ada wakizingatia hali halisi ya mishahara ya wauguzi, kodi na makato na waone busara kama ipo haja na hoja ya kuongeza ada hiyo.

“Suala hili ni hoja ya walio wengi, ninyi nyote mmemuona Mhe. Rais akizungumzia kuondolewa kwa tozo nyingi zisizo na sababu kwenye kilimo, mifugo, uvuvi; hata hili la kwenu linaweza kusababisha serikali iwe na nia ya kufahamu mabaraza yake yote na tozo zao, nawaomba viongozi mlitafakari muone kama ipo hoja na haja ya kuongeza gharama za ada,” alisema Mtaka.

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema mkoa unatambua kazi inayofanywa na wauguzi  ya kutoa elimu kwa wajawazito nakuhamasisha wajifungulie  kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo mwaka 2017 wanawake waliojifungulia kwenye vituo vya afya ni asilimia 55 na mwaka 2018 ikapanda kufikia  asilimia 70.

Naye Afisa Muuguzi kutoka Halmashauri ya Ubungo Bi. Aliho Ngeregenza amesema  wauguzi walio wengi vipato vyao wanavyopata haviendani na gharama za leseni wanazolipia hivyo ombi lao wapunguziwe gharama hizo

Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara ambalo linahusisha wauguzi zaidi ya 800 litafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/wauguzi-waomba-ada-ya-leseni-za-uuguzi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa