Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ulinzi wa hifadhi za Taifa ni pamoja na kutoruhusu mifugo kuchungiwa kwenye hifadhi ili hifadhi hizo endelevu kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara pamoja na washiriki wa Mbio za Serengeti Safari Marathon kutoka mikoa mbalimbali nchini na wengine kutoka nje ya nchi na nje ya bara la Afrika zilizofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
“Mikoa miwili ya Simiyu na Mara tu ina ng’ombe zaidi ya milioni tano, tukisema turuhusu mifugo ichungiwe kwenye hifadhi hakuna mnyama atakayebaki na hapo hakutakuwa na hifadhi tena hili siyo suala la kisiasa; sisi viongozi wa kisiasa tukilipigia siasa jambo hili hiyo sifa tunayoisema ya Serengeti kuwa Hifadhi ya kwanza Duniani haitakuwepo baada ya kuruhusu ng’ombe kuingia kwenye hifadhi,” alisema Dkt. Kikwete.
Aidha, Dkt. Kikwete amewapongeza waandaaji wa Serengeti Safari Marathon kwa namna kwa kuanzisha mbio hizo ambazo zao jipya la utalii ambayo ikitangazwa vizuri itatangaza utalii nchini na kuweza kulifikia lengo la serikali la kufikisha watalii 5,000,000 ifikapo 2025 kutoka 1,300,000 wa sasa, huku akitoa wito kwa wadau wa utalii kujenga hoteli kwa ajili ya kuwapokea wageni/watalii.
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/11/watanzania-tumuunge-mkono-jpm-kulinda.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa