Viongozi na wanachama wa Vyama vya Ushirika wa Mazao -AMCOS Mkoani SIMIYU wamesema chanzo cha wakulima wa Pamba kuchanganya mchanga na mafuta ya kenge kwa madai ya kuongeza uzito katika zao hilo kinatokana na baadhi ya wanunuzi wasio waaminifu kuwaibia kupitia mizani.
Hayo wameyasema katika majadiliano ya namna ya uendeshaji vya Vyama vya Ushirika na uanzishwaji wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa SIMIYU mjadala ulioandaliwa ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini.
Kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka na viongozi na wanachama wa Vyama vya Ushirika wa Mazao -AMCOS chenye lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wakulima na uanzishwaji wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa SIMIYU.
Katika mjadala huo wadau hao wamesema udangangifu katika mizani ya kupima uzito wa Pamba umechangia kwa kiasi kikubwa wakulima kutumia mbinu mbadala za kuongeza uzito
Moses Masalu Mwenyekiti wa chama cha ushirika mhango halmashauri ya mji wa bariadi amesema kuwepo kwa wizi wa pamba katika mizani za kupimia uzito kumesababisha wakulima wengi kutumia mbinu mbadala za kuongeza uzito ili kufidia machungu ya kuibiwa pamba yao na makarani wanapoenda kuuza pamba.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amesema kuchelewa kuanza kwa msimu wa pamba kunachangia kushuka kwa bei soko la dunia kutokana na kugongana na mataifa mengine katika msimu na hivyo kupendekeza kuanza april badala ya mei na juni.
Kwa upande wake Kaimu Mrajisi Masoko na Uwekezaji Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, EDMUND MASSAWE amesema nia ya serikali ya kuimarisha ushirika nchini ni kuviwezesha vyama vikuu kununua mazao ya wakulima.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amewasisitiza viongozi wa vyama hivyo kuwa waadilifu .
Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa SIMIYU kinatarajiwa kuundwa April mwaka huu kabla ya kuanza msimu wa ununuzi.
KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII BONYEZA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/01/wanunuzi-wa-pamba-wasio-waaminifu.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa