• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wanawake Watakiwa Kuwalinda Watoto wa Kike Dhidi ya Mimba za Utotoni

Posted on: March 8th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga ametoa wito kwa wanawake  wote Mkoani Simiyu kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda watoto wa kike na kuhakikisha hawakatishwi masomo kwa sababu ya kupewa mimba wakiwa (katika umri mdogo) shuleni na badala yake wamalize masomo ili watimize ndoto zao.

Kiswaga ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na wanawake wa Mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka,  katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mjini hapo.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imetoa fursa kwa watoto wote kupata elimu bila malipo hivyo wazazi hususani wanawake (wakinamama) wanapaswa kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha wanawasaidia watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia mienendo yao na kuwaonya wanapoenda kinyume  ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Endapo mama kwenye familia atatimiza wajibu wake wa kumwangalia na kumwonya mtoto wa kike kuachana na vitendo vitakavyopelekea kupata mimba,  huyo mtoto atakuwa salama; kwa hiyo wakinamama timizeni wajibu wenu wa kuhakikisha mnawalinda watoto wa kike kama walivyofanya wazazi wetu zamani ili waweze kumaliza shule salama” alisema Kiswaga.

Ameongeza kuwa  wazazi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kuwafichua wanaume wote waliowapa mimba wanafunzi wa kike na kuhakikisha wanafikishwa katika vyombo vya dola ili waweze kuchukuliwa hatua badala ya kuwa upande wa wahalifu hao na kuwatetea.

Katika hatua nyingine Kiswaga ameziagiza Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kwamba zinatekeleza maagizo ya Serikali katika kutenga asilimia 10 kwa ajili ya wanawake na vijana na kuzitoa kama ilivyokusudiwa ili kuyasaidia makundi hayo kupata mitaji kwa ajili ya kuendeshea shughuli mbalimbali  za kuwaingizia kipato.

Aidha, ametoa wito kwa wanawake wa Mkoa wa Simiyu kuunga mkono juhudi za Serikali Mkoani humo katika uanzishwaji wa viwanda vidogo ili kutekeleza kwa vitendo Mkakati wa  Mkoa wa “Wilaya Moja Bidhaa Moja”, kwa lengo la kuwezesha kujitegemea kiuchumi na kuondokana na utegemezi kwa wanaume.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu Mariam Manyangu amewataka wanawake wa Mkoa huo kufanya kazi kwa bidii na  kujiamini katika majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa Mkoa wa Simiyu, Mwenyekiti wa Maandalizi ya Siku ya Wanawake mkoani SIMIYU, Mwl. Rachel Ernest amesema Wanawake Mkoani humo wanalaani vitendo vya baadhi ya watu katika jamii kuendelea kumtumia mtoto wa kike kama kitega uchumi kwa tamaa ya kupata ng’ombe, hivyo kumkatisha masomo ili aolewe na kushindwa kutimiza ndoto za maisha yake .

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2018 yameadhimishwa chini ya Kauli Mbiu isemayo “Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tuelimishe Usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini”,   ambapo wanawake mkoani Simiyu walianza maadhimisho hayo kwa kwenda kuwaona wagonjwa(wanawake na watoto) katika Hospiitali Teule ya Mkoa wa Simiyu na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni na vinywaji.

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/03/wanawake-watakiwa-kuwalinda-watoto-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa