Jumla ya Wananchi 17,084 wa kata ya Igalukilo na Vijiji jirani wilayani Busega wanatarajia kunufaika na huduma za vipimo mbalimbali vya afya na kupunguza umbali wa kupata huduma hiyo mara baada ya kukamilika kwa Jengo la Maabara linalojengwa katika Kituo cha Afya cha Igalukilo
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega, Dkt. Godfrey Mbangali wakati akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa jengo hilo kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo.
Pamoja na Jengo hilo Mwenge wa Uhuru umepitia miradi mbalimbali wilayani Busega ikiwa ni pamoja na Vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo Shule ya Sekondari Ngasamo, ujenzi wa Jengo la Benki ya NMB na Ujenzi wa Kisima Kirefu cha Maji Kijiji cha Bukabile.
Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 amekagua kazi zinazofanywa na vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu pamoja na kuzindua klabu ya Wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Kabita.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/wananchi-17084-kunufaika-na-huduma-za.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa