• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi Zaidi ya 1000 Wapatiwa Msaada wa Kisheria Mkoani Simiyu

Posted on: October 25th, 2019

Msajili wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Felistas Mushi amesema  takribani wananchi 1018  wamepata huduma ya msaada wa kisheria katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria tangu Oktoba 21, 2019 mpaka Oktoba 25, 2019, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mushi ametoa taarifa hiyo katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Oktoba 25, 2019 ambapo amebainisha kuwa asilimia kubwa ya matatizo ya kisheria yalihusu migogoro ya ardhi na yameshafikishwa mahakamani  na yako katika hatua mbalimbali.

Amesema huduma walizopata wananchi katika wiki ya msaada wa kisheria ni pamoja na huduma za usuluhishi, ushauri wa kisheria, kuandaa nyaraka na maelekezo ya sehemu  sahihi ya kwenda pindi wanapopata migogoro.

“Mbali na huduma kwa wananchi mafunzo yametolewa kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma wapatao 1300 wakiwemo, wajumbe wa menejimenti ya sekretarieti ya mkoa, wajumbe wa kamati ya parole, wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji, wajumbe wa kamati ya maadili ya mahakimu, askari polisi na magereza, wajumbe wa kamati za shule na watendaji wa vijiji na kata, “ alisema Mushi.

Kwa upande wake Hakimu Mary Nyangusi akimwakilisha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio, ametoa wito kwa wananchi kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo mingi inatokea mara nyingi wanaume( baba) wanapofariki na wake(mke) na watoto kudhulumiwa haki zao.

Adam Kisinza ni Mmoja wa wananchi waliofika kupata msaada wa kisheria katika maadhimisho hayo amesema, “nashukuru nimeelewesha ninachotakiwa kufanya maana kule kwetu baba mwenye mji anapokuwa amefariki wakabaki watoto na mama, wanakuwa hawana mamlaka juu ya mali iliyoachwa maana kila mtu anataka achukue chake wakati mzee hakuacha hata  wosia”.

Akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema wizara ya katiba na sheria ikaona umuhimu wa kupeleka maadhimisho ya wiki ya msaada wa huduma za kisheria katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, ili wananchi wapate uelewa wa masuala ya kisheria na kupata matokeo yatakayoonekana

Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Kitaifa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu:- “Msaada wa Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”ambapo kilele cha maadhimisho haya kimeenda sambamba na uzinduzi wa Jarida la Msaada wa Kisheria, ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KATIKA TUKIO HILI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/wananchi-zaidi-ya-1000-wapata-msaada-wa.html


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa