Meatu,
Wananchi Mkoani Simiyu wametakiwa kutowanyanyapaa na kuwakimbia wagonjwa watakaokutwa na magonjwa ya kuhara na badala yake wameshauriwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu wakati wa utoaji wa huduma ya kwanza sambamba na utoaji Taarifa mapema ili kunusuru uhai wa wagonjwa.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Afya Mkoa wa Simiyu Bw.Bashiru Salum katika kikao cha kujadili mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
Ameeleza kuwa kuwapa huduma ya kwanza kwa wakati wagonjwa watakaobainika kuwa na dalili za kipindupindu itasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ulipuko wa magonjwa hayo kuenea maeneo mengine.
Aidha ametoa rai kwa wataalamu kuelekeza nguvu kubwa katika utoaji wa Elimu kwa Jamii juu ya namna bora ya utoaji wa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wenye dalili za magonjwa ya kuhara hatua itakayosaidia kudhibiti kuenea kwa ugonjwa na pia kuokoa Maisha ya wagonjwa.
Licha ya kutokuwepo kwa kisa chochote cha magonjwa ya kuhara Wilayani Meatu,wataalamu wa Afya Wilayani humo wamehimizwa kujikita zaidi katika utoaji wa Elimu ya kujikinga na magonjwa hayo.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa