• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi wapiga kura za siri kubaini Watuhumiwa wa Mauaji ya watoto Busega

Posted on: February 14th, 2019

Wananchi wa Kata ya Lamadi Wilayani Busega mkoani Simiyu wamepiga kura za siri kwa lengo la kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo.

Wakizungumza katika zoezi hilo lililofanyika Februari 14, 2019  katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi wananchi hao wamesema kuwa  wamelipokea vizuri zoezi hilo na kubainisha kuwa kura hizo zitasaidia Vyombo vya Dola katika kufanya uchunguzi na kuwabaini wauaji wa watoto wilayani humo.

“Zoezi hili nimelipokea vizuri na nina imani litatusaidia kuwapata wauaji wa watoto wetu na naishukuru Serikali kuona haja ya kuwashirikisha wananchi maana mauaji haya ya watoto yametusikitisha sana wakazi wa Lamadi” alisema Modesta Andrea mkazi wa Lamadi

“ Tukio hili la kupiga kura za siri mimi naona ni zuri kwa sababu naamini kuna baadhi ya wananchi wanaweza wakawa wanafahamu watu waliofanya mauaji ya watoto na kama ikitokea kuna watu wakaandikwa labda kwa sababu ya fitina tunaamini vyombo vyetu vya dola vitachuja na kuchunguza na mwishowe wauaji watabainika tu; tunaomba wakibainika sheria ifuate mkondo wake” alisema Elisha Daniel mkazi wa Lamadi.

Akizungumza na wananchi wa Lamadi mara baada ya zoezi hilo kukamilika, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema kufanyika kwa zoezi hilo hatua ya kwanza ya uchunguzi wa mauaji ya watoto wilayani humo, huku akiwahakikishia wananchi kuwa kura walizopiga zitahesabiwa kwa haki na vyombo vya dola mkoani humo.

“Kupiga kura za siri si kwamba tumeshindwa kufanya upelelezi, hii ni hatua ya kwanza ya sisi kufanya uchunguzi wetu, kura hizi zitahesabiwa na vyombo vya dola mkoani Simiyu ambavyo ni Usalama wa Taifa, Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Jeshi la Wananchi JWTZ (Mkoa wa Simiyu), Jeshi la Zimamoto, Jeshi la Polisi na TAKUKURU” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema Serikali mkoani humo itaendelea kutimiza wajibu wake wa kwanza wa kulinda watu wake na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani ili waweze kufanya vema shughuli za maendeleo.

Sambamba na hilo Mtaka amesema Serikali itahakikisha inayafanyia kazi masuala mbalimbali yaliyosemwa na wananchi katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na malalamiko dhidi ya utendaji wa baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali  na kubainisha kuwa  hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaobainika kwenda kinyume katika kuwatumikia wananchi.

“Niwahakikishie kuwa Serikali itayafanyia kazi yote yaliyosemwa na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hapa Lamadi, kama kuna wakubadilishwa watabadilishwa, wa kuwajibishwa watawajibishwa, wakuhamishwa watahamishwa naomba mniamini” alisisitiza Mtaka.

Kwa upande wake Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni ametoa pole kwa wazazi wote waliopoteza watoto wao katika mauaji ya watoto na kuahidi kutoa rambirambi shilingi 500,000/= kwa kila familia iliyokutwa na msiba huku akilaani vikali vitendo vya mauaji ya kinyama ambayo yamekatisha ndoto za watoto hao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera amewashukuru wananchi wa Lamadi kwa  namna walivyojitokeza katika zoezi la kupiga kura za siri na kwa namna walivyolifanya kwa amani na utulivu.

MWISHO

 

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/02/wananchi-wapiga-kura-za-siri-kubaini.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa