Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho amewahimiza wananchi wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi linalotokana na utekelezaji wa Sera ya Elimu bila malipo.
Kabeho ametoa wito huo katika kijiji cha Jija wakati akizindua mradi wa Maji na vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Jija, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 19, 2018 .
Amesema kutokana na utekelezaji wa sera ya Elimu bila malipo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa darasa la awali, darasa la kwanza wanaojiunga na kidato cha kwanza, hivyo wananchi wawekeze katika ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine ya elimu ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.
Katika hatua nyingine Kabeho amewataka Watumishi wa Umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa kwa weledi na ufanisi mkubwa wakiizingatia sheria, kanuni na taratibu.
“Mhe. Rais anaposema HAPA KAZI TU anamaanisha fanya kazi kwa bidii, zingatia sheria, taratibu na kanuni, wapo watumishi wanafanya kazi pale tu palipo na maslahi mahali ambapo hapana maslahi hamwajibiki, achaneni na kufanya kazi kwa mazoea fanyeni kazi kwa kujituma na kwa ufanisi” alisema
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki akizungumza kwa niaba wa wananchi ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kuwaletea wananchi maendeleo, ambapo ameshukuru kwa kupelekea miradi hiyo ya maji na elimu katika Kijiji cha Jija ,huku akisisitiza wazazi kutowakatisha masomo watoto wao hususani wa kike.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Maswa umepitia miradi yenye thamani ya milioni 516, inayotoka katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Maendeleo ya Jamii (Vikundi vya vijana na wanawake)
Mbio za mwenge mkoani SIMIYU zimehitimishwa Agosti 19 baada ya kuanza kukimbizwa Agosti 14 ukitokea mkoani Singida na unatarajiwa kukabidhiwa mkoani Shinyanga Agosti 2018.
MWISHO
PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-http://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/wananchi-simiyu-wahimizwa-kuwekeza.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa