Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka amewasisitiza wakulima Mkoani humo mazao ya biashara yenye tija hasa zao la pamba kwa kuzingatia Mkoa huo upo katika mchakato wa utekelezaji wa ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na zao la pamba.
Msisitizo huo ameutoa jana Wilayani Maswa katika ziara yake ya kuhamasisha kilimo kuelekea msimu wa kilimo mwaka 2017/2018 na kueleza kuwa wakulima wanapaswa kuutumia vema msimu huu kwa kulima zao la pamba ambalo litawapatia fedha nyingi.
Mtaka alieleza kuwa wakulima wa Maswa na Mkoa mzima wageuze ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za afya kuwa ni fursa ya kujiongezea kipato kwa kuzalisha zaidi zao la pamba ambalo ndilo litakuwa malighafi kuu katika uzalishaji wa kiwanda hicho.
Aidha alisema katika msimu msimu huu mpya wa mwaka 2017/2018 wakulima hao wanatakiwa kuondoa mazalia ya pamba yaliyobaki mashambani mwao na kisha kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo hicho.
"Katika msimu huu ninawaomba wakulima wote waondoe mazalia ya zao la pamba yaliyobaki mashambani kwa kuyachoma moto ili wasije kuharibu na kuambukiza magonjwa katika mbegu mpya na bora watakazozitumia...pia katika kupanda mpande kwa kuzingatia sentimeta 90 hadi 40 zilizoainishwa kitaalamu kutoka mstari hadi mstari....alisema Mtaka
Aidha wakulima hao hawakusita kueleza kero zao na kuitupia lawama bodi ya pamba kwa kushindwa kusimamia zao hilo huku wakidai kutoichafua kwa kuweka maji na mchanga katika zao hilo.
Irene Joseph mkulima kutoka katika kata ya Kadoto alifafanua kuwa wakulima wamekuwa wakionewa na kusingiziwa visingizio vingi juu ya uchafuzi wa zao hilo ,huku akieleza tuhuma hizo kuwa si za kweli na kubainisha kuwa bodi ya pamba inapaswa kutimiza wajibu wake katika kulisimamia zao la pamba na kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima .
Nae afisa kilimo wa Wilaya ya Maswa Christopher Simwimba amewataka wakulima kutumia mbolea ya samadi katika kuongeza rutuba kwenye mashamba yao .
Afisa huyo aliongeza kusema kuwa wakulima wanatakiwa kubadilika na kulima kisasa ili waweze kuendana na falsafa ya serikali ya viwanda ambapo wakulima ndio wanategemewa wao kuwa ni wazalishaji wa malighafi za viwandani.
Nae mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt Seif Shekilage alisema kuwa katika kuhakikisha wanaboresha na kuliinua zao la pamba Halmashauri yake imeweza kuwasaidia vikundi vya vijana na wanawake wanajihusisha na kilimo kuwapatia mkopo wa Milioni 50 kwa vikundi 16 vinavyotarajia kulima zao la pamba kwa msimu huu.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dk Seif Shekalage akitoa ufafanuzi wa namna Wilaya yake ilivyojipanga kuongeza uzalishaji wa zao la pamba.
Wakulima kutoka katika kata 36 za Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu wakiwa katika mkutano wa pamoja Viongozi wa Mkoa na Wilaya(hawapo pichani) ukiwa na lengo la kujadili na kupokea maelekezo ya kilimo katika msimu mpya wa 2017/2018.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa