• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi Mkajiandikishe, Mchukue Fomu Na Kupiga Kura Uchuguzi Serikali Za Mitaa: RC Mtaka

Posted on: October 7th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthnony Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa mkoani hapa kwenda kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura, kugombea nafasi mbalimbali na hatimaye kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019  ili wapate viongozi waadilifu.

Mtaka ametoa wito huo  wakati akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu, baada ya ibada ya misa takatifu Oktoba 06, 2019 ambapo alibainisha kuwa wananchi wanapaswa kuchagua viongozi waadilifu na wacahapakazi ambao watasimamia vizuri fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

“Kuanzia tarehe nane mwezi huu uandikishaji unaanza nendeni mkajiandikishe na wote wenye sifa chukueni fomu za kugombea nafasi mbalimbali  na kujitokeza kupiga kura siku ya tarehe 24 Novemba ili mpate viongozi bora, tumekuwa tunapata migogoro mingi ya ardhi, fedha za miradi kutotumika inavyotakiwa na moja ya sababu ni vongozi wasio waadilifu, kajitokezeni mchague waadilifu, “ alisema.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu kusomesha watoto wao  na kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo vyumba vya madarasa na mabweni ambayo yatawapunguzia watoto wa kike kutembea mwendo mrefu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi wilayani Meatu, Paroko Robert Walwa amesemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kusisitiza umuhimu wa kupenda elimu jambo ambalo amesema hata Biblia Takatifu imesisitiza kuishika elimu maana ndiyo chimbuko la imani,  hivyo  ni vema wananchi wakazingatia elimu ili imani zao ziimarishwe.

Naye mmoja wa waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Mwanhuzi aliyejitambulisha kwa jina moja la Jennifer amesema wananchi wanamshukuru Mkuu wa Mkoa kwa jitihada anazozifanya katika mkoa ambazo zimekusudia kuinua mkoa kielimu na akabainisha kuwa watashirikiana na Serikali katika kuhakikisha malengo ya kuinua sekta ya Elimu yanatimia ikiwemo kuongeza ufaulu.

Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Bi. Jeniffer amesema atahakikisha anajiandikisha na kupiga kura siku ikifika ili aweze kutumia vema haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi anayemtaka na si wa kuchaguliwa na watu wengine.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/mkuu-wa-mkoa-wa-simiyu-mhe.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa