RC DKT.NAWANDA ATHIBITISHA MAANDALIZI KUKAMILIKA KWA ASILIMIA 100,
AMSHUKURU RAIS DKT.SAMIA KWA KUTOA BILIONI 36.2 KUTEKELEZA MIRADI YA ELIMU KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.
Bariadi,
Jumla ya Wanafunzi 33,784 wanatarajiwa kuripoti kidato cha kwanza kwa ajili ya kuanza muhula mpya wa masomo ifikapo Tarehe 8 Januari 2024 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.Dkt Yahaya Esmail Nawanda ameeleza.
Ameeleza hayo katika kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Mohamed Mchengerwa na Wakuu wa Mikoa kilichofanyika kwa njia ya Mtandao 30 Disemba 2023 katika ukumbi wa mikutano Ofisini kwake.
Dkt Nawanda amemhakikishia Waziri Mchengerwa kuwa Maandalizi ya Wanafunzi hao yamekamilika kwa Asilimia Mia moja na kwamba Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa ajili ya muhula mpya wa Masomo wataripoti katika Shule 177 zilizokamilika.
Aidha Mkuu wa Mkoa Dkt.Nawanda ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Fedha Bilioni 36.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika Sekta ya Elimu ndani ya Mkoa wa Simiyu katika kipndi cha Mwak wa Fedha 2023/2024.GCO,Simiyu RS,30 Disemba 2023.
GCO,
Simiyu RS,
31 Disemba 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa