• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wanafunzi 19,242 Wachaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2018 Mkoani Simiyu

Posted on: December 8th, 2017

Jumla ya wanafunzi 19,242 mkoani Simiyu sawa na asilimia 92.5 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari katika awamu ya kwanza kwa mwaka 2018.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini katika kikao cha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha  kwanza mwaka 2018 kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Sagini amesema jumla ya wanafunzi 20,818 sawa na asilimia 67.73 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walifaulu, ambapo kati yao 1576 sawa na asilimia 7.5 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuanza kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika baadhi ya Halmashauri.

“Wanafunzi waliokosa nafasi Halmashauri ya Mji wa Bariadi ni wale waliopaswa kwenda Shule ya Sekondari Kidinda(207) na Biashara(162), Halmashauri ya Wilaya ya Busega walipaswa kwenda shule za Lamadi (486), Nasa (358) na Sogesca (363). Ni wajibu wa Halmashauri hizi kushirikiana na wananchi kuhakikisha miundombinu pungufu imekamilishwa haraka ili ifikapo Februari 15, 2018  wanafunzi hao waripoti kwenye shule walizopaswa kwenda” amefafanua Sagini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Halmashauri ya Mji Braiadi wamesema Halmashauri zao zinaendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa na wataendelea kufanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha kuwa miundombinu hiyo pungufu inakamilika haraka, ili kufikia Februari 05 mwakani wanafunzi wote waliokosa nafasi awamu ya kwanza waweze kwenda shule.

Wakati huo huo Sagini amezitaka Halmashauri kuendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018 bila vikwazo vya aina yoyote.

Ameongeza kuwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla washirikiane na uongozi wa wilaya, halmashauri na shule  kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa, wanaripoti shuleni na kuendelea na masomo yao kwa bidii hadi watakapomaliza elimu yao ya sekondari mwaka 2021.

Akielezea hali ya ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba  kwa mwaka 2017, Afisa Elimu Mkoa, Mwl. Julius Nestory amesema kwa mara ya kwanza mwanafunzi aliyeongoza katika Mkoa ambaye ni (msichana) Hoka Lyaganda Saguda ametoka katika Shule ya Serikali ambayo ni Shule ya Msingi Sima B iliyopo Mjini Bariadi.

Amesema ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu na kuinua kiwango cha ufaulu mkoani humo Mikakati ya kuinua ufaulu ya kila wilaya isimamiwe kikamilifu,  Ofisi za Wilaya, Halmashauri, Kata na Wakuu wa Shule zifanye ufuatiliaji kuhusu ufundishaji na ujifunzaji na  Ukaguzi wa shule ufanyike kwa kiwango kisichopungua asilimia 50 kwa mwaka na Wakurugenzi watenge fedha kwa ajili ya ukaguzi wa shule.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mhe.Mahamoud Mabula ameshauri kuwa ili kuinua ufaulu suala la maendeleo ya Elimu liwe agenda ya kudumu katika vikao vyote muhimu vya Halmashauri mkoani humo, ili kutoa nafasi ya kujadili changamoto mbalimbali za sekta ya elimu na kuzitafutia ufumbuzi.

Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu imeongezeka kutoka wanafunzi 16,620 mwaka 2017 hadi wanafunzi 19,242.

Afisa Elimu Mkoa, Mwl. Julius Nestory akiwasilisha taarifa ya hali ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka 2017, katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wiayaya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akichangia hoja katika katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo  Mjini Bariadi.

Katibu Tawala Wilaya ya Meatu, Veronica Kinyemi akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika Mjini Bariadi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Anderson Njiginya, akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhandisi Paul Jidayi akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo Mjini Bariadi

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mahamoud Mabula akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

:-Mkurugenzi wa Mji wa Bariadi, Ndg.Melkezedeck Humbe akichangia hoja katika  kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, kilichofanyika leo Mjini Bariadi

Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa