• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waliopata Sifuri Mtihani wa ‘Mock’ Kidato cha Nne Simiyu Kuwekwa Kambi Maalum ya Kitaaluma

Posted on: August 22nd, 2019

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa katika kambi maalum ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri  kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu na kufikia  daraja la nne na kuendelea,  katika mtihani wa Taifa mwaka huu 2019.

Mtaka ameyasema hayo Agosti 22, 2019  katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa wanafunzi wa kidato cha nne na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi bora Kitaifa.

Mtaka amesema lengo la Mkoa ni kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna mwanafunzi wa kidato cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye daraja sifuri na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja na kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata ufaulu mzuri.

“ Tutaweka kambi ya wanafunzi wote waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata wale waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye sifuri, Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu, Civics(Uraia), Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D ili wapate cheti; nia yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya vizuri" alisema

Katika hatua nyingine Mtaka amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu ufundishaji na kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa Taifa wa Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018 kwenda kwenye nafasi nzuri zaidi.

Afisa elimu wa mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata na wilaya  kuendelea kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya vizuri na wale ambao shule zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi ili kuongeza ufaulu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa Mock ambao wapo takribani  2000 kati ya wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada kwao na wanatarajia kuzifanya kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single digit).

Mkuu wa mkoa ameahidi kutoa shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora kitaifa, Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na milioni mbili kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu daraja la kwanza pointi saba na kuwa katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa atapewa shilingi milioni moja.

Mkutano wa tathimini ya matokeo ya kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa shule za sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri lengo likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya elimu mkoani Simiyu

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/08/mkuu-wa-mkoa-wa-simiyu-mhe.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa