• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wakurugenzi watakiwa kuzingatia Afua za Lishe katika Bajeti za Halmashauri kukabiliana na Udumavu kwa watoto

Posted on: November 13th, 2018

Kuelekea katika kipindi cha maandalizi ya  bajeti ya mwaka 2019/2020 wito umetolewa kwa  Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu na maeneo mengine kote nchini kuyapa kipaumbele masuala ya Lishe katika mipango na bajeti za Halmashauri zao, ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele wakati mafunzo maalum yaliyotolewa kwa baadhi ya viongozi na maafisa Lishe, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.

Kihwele amesema takribani asilimia 34 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima wana udumavu, hivyo ipo haja ya kutilia mkazo suala la lishe ili kutoathiri maendeleo ya ukuaji wa watoto, uwezo wao wa kufikiri na maendeleo yao kitaaluma(shuleni).

“Asilimia 34 ya watoto wa  nchi nzima wenye umri chini ya miaka mitano wana utapiamlo, suala hili linaathiri sana watoto, mfano matokeo yao shuleni na uwezo wa kufikiri, ndio maana serikali imeweka lishe kama kipaumbele na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama wasimamizi tunapita kwenye Halmashauri nchi nzima kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya lishe katika bajeti ya mwaka 2019/2020” alisema

Ameongeza kuwa katika mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Viongozi pia yamelenga  kuwakumbusha juu ya utekelezaji wa vipengele vya mikataba ya afua za lishe iliyosainiwa katia ya  Wakuu wa Mikoa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na kutenga shilingi 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano katika bajeti zao.

Naye Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa ametoa wito  kwa Halmashauri kutenga  fedha kwa ajili ya masuala ya lishe kwa kuzingatia miongozo na kuhakikisha fedha zinazotengwa zinatumika katika shughuli zilizopangwa ili kuondokana na tatizo la utapiamlo

Aidha, Bi. Mariam amesema pamoja na kukabiliana na tatizo la utapiamlo fedha hizo zielekezwe katika huduma za utoaji wa virutubisho vya nyongeza kama vile virutubisho vya Vitamini A na vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa akina mama wajawazito.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini aliwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu kuyachukulia masuala ya lishe kama kipaumbele, huku akiwataka kuhakikisha wanafanya vikao vya kamati za lishe za wilaya kila baada ya miezi mitatu kama ilivyoanishwa  katika miongozo.

Diwani wa Kata ya Dutwa Mhe.Mapolu Mkingwa akizungumza kwa niaba ya  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba amesema maelekezo na mafunzo waliyoyapata watayapelekea katika Mabaraza ya madiwani na kuhakikisha mipango na bajeti zinazopitishwa zinazingatia umuhimu wa afua za lishe.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesisitiza viongozi na watendaji wakiwemo wajumbe wa kamati za lishe kubadilika na kuachana na mazoea katika kufanya ufuatiliaji na kutekeleza mipango ya masuala ya lishe badala yake wafanye kazi kulingana na miongozo ili kuwa na matokeo mazuri katika masuala ya lishe.

Timu ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ipo katika ziara ya kuhamasisha Viongozi katika Halmshauri na Mikoa kuzingatia vipaumbele kwenye maeneo ya lishe na kupanga mipango ya bajeti inayojibu changamoto za lishe, ili kufikia malengo ya  mikataba ambayo Wakuu wa Mikoa walisaini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenye usimamizi wa afua za lishe katika maeneo yao.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/11/wakurugenzi-watakiwa-kuzingatia-afua-za.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa