• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wakandarasi Tekelezeni Miradi ya Maji kwa Uadilifu na kwa Wakati

Posted on: December 22nd, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amewataka Wakandarasi na Local fundi wa miradi ya maji mkoa wa Simiyu  kutekeleza miradi ya maji kwa uadilifu na wakati. Mhe. Kafulila ameyasema hayo wakati wa hafla ya kusaini mikataba 24 kati ya RUWASA na wakandarasi na RUWASA na Local Fundi.

Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa RUWASA- Simiyu Eng. Mariam Majala amesema kuwa baada ya kuanzishwa kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini,mkoa wa Simiyu unaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji 53 katika Wilaya za Busega, Meatu, Maswa, Itilima na Bariadi, aidha kati ya miradi 53, miradi 31 ni mipya, miradi 10 ya upanuzi, miradi 9 ya ukarabati na miradi 3 ya ukamilishaji. Eng Mariam ameeleza kuwa miradi yoye hiyo 53 inatekelezwa kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account).

Akieleza kuhusu usainishaji wa mikataba mipya 24, Eng.Mariamu ameeleza kuwa "Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) leo tunatarajia kutia saini ya mikataba 24 kati ya 36 yenye gharama ya Tsh. 6.9bln. Mikataba 12 ni ya Wakandarasi na mikataba 12 ni ya Local fund. Aidha mikataba ya miradi 4 inatarajiwa kusainiwa na RUWASA makao makuu na mikataba ya miradi 8 itasainiwa katika awamu ya pili mara baada ya taratibu za ununuzi kukamilika". Meneja RUWASA Simiyu amebainisha kuwa mikataba yote iliyosainiwa 22/12/2021 itafanya kazi kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari, 2022 hadi June 2022. Baada ya kukamilika kwa miradi hiyo Mkoa wa Simiyu unatarajia kuongeza vituo vya kuchotea maji 143 ambavyo vitahudumia wananchi wapatao 35,750 na kufanya idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama kwa maeneo ya vijijini mkoani humo kufikia 1,185,035 sawa na asilimia 73.6. 

Akizungumza, changamoto zinazowakabili Watanzania,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, ameeleza kuwa utafiti uliofanywa 2008 kupitia kura za maoni,ulionyesha kuwa kati ya matatizo makunbwa manne yanayowasumbua Watanzania, tatizo la pili lilikuwa maji, wakati tatizo la nne likiwa rushwa.Hii inaonyesha kuwa suala la maji ni suala ni suala muhimu sana. Hivyo uamuzi wa kuanzisha RUWASA ulikuwa uamuzi sahihi. 

 Mkoa wa Simiyu una idadi ya watu wapatao 1.9ml, kati ya hao ni watu 1.14 mln sawa na 67.22% ndio wanaopata maji safi na salama. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 ongezeko la upatikanaji wa maji ni lita 1,833,400 sawa na 6.4%. Ni imani yangu kuwa kwa kusaini hii mikataba ya miradi 24 yenye thamani ya 6.9bln.Upatikanaji wa maji katika mkoa wa Simiyu utaongezeka kutoka 67.22% kufikia 73.6%.Lengo letu ni kufikia 85%.Hali hii inaonyesha waziwazi kuwa fedha za maji sio tatizo bali utekelezaji ndio mgogoro.

 "Wito wangu kwa wakandarasi na Local Fundi, tekelezeni miradi hii kwa uadilifu na kwa wakati.Kwani kwa kufanya kazi kwa wakati au hata chini ya wakati na kwa ubora mtakuwa mmejitangaza zaidi. Halmashauri taarifa kuhusu masuala ya maji, umeme, Pamba,ni taarifa muhimu kwenye vikao na ziwe zinatolewa kwenye kila kikao cha madiwani. Madiwani wanatakiwa kuwa nazo, na hii itaongeza umaarufu wa RUWASA". Amesisitiza Mhe.Kafulila.

 Maji ni kitu muhimu sana katika mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu.Miaka miwili iliyopita upatikanaji wa maji Mkoani Simiyu ulikuwa 40.5%, Kufikia June 2022 upatikanaji wa maji Simiyu utakuwa 73.6%. Hii inaonyesha wazi kuwa tunaweza tukafika zaidi ya 90%. Pongezi kwa kazi nzuri mnayofanya RUWASA. Hongera Meneja RUWASA kwa uwazi. Hii inaongoza uwajibikaji. Ni imani yangu kuwa upatikanaji wa watoa huduma ulizangatia mchakato,sheria, kanuni na taratibu.Hivyo nendeni mkapige kazi na kazi iwe kwenye moyo na kiganja chako.

 Kwenye hii Tsh.6.9bln,toeni hata misaada kwa jamii (CSR) kwani nyie ni wawekezaji. Mkalipe Kodi  zote mnazotakiwa kulipa kwa mujibu wa sheria hii ni pamoja na Service levy,malipo ya service levy yalipwe kwa Halmashauri husika.Ushuru ni vitu ambayo vipo kisheria na vilipwe. Simiyu ni yetu pamoja hivyo ni lazima tuijenge.Nawakumbusha wajibu wenu na muende mkatende, kafanyeni kazi.Lengo ni moja kumtua mama ndoo kichwani.

Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed, aliwapongeza RUWASA kwa kazi nzuri na kuwakumbusha wakandarasi na Local Fundi kuwa kazi waliyopewa ni ya miezi 6 tu."Kama Chama tutaanza kukagua miradi yote mwezi 3.Miradi hii ikamilike kwa wakati. Ni matarajio yetu kuwa kama ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya chama kuwa ili ifikapo 2025, 85% ya watu wote kutumia maji safi na salama itimie

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Njalu Silanga, amesema, kikao hiki kimehusisha Waheshimiwa wabunge, viongozi wote wa Chama na Serikali, hivyo makandarasi kumbukeni kwamba mmesaini mikataba mbele yetu na tunatarajia mtafanya kazi vizuri, tutawapa ushirikiano, hatuhitaji malalamiko, tunataka kazi ifanyike.

Aidha, Mbunge wa Meatu Mhe. Leah Komanya, alitoa shukrani kwa tukio hili la usainishaji mikataba kwani ni la mara ya kwanza na kubwa zaidi yote mikataba 24 kusainiwa Mara moja. Mhe.Komanya aliwafahamisha washiriki wa hafla hiyo kuwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais alianzisha kampeni ya kumtua mwanamke ndoo kichwani, kampeni ambayo akiwa Rais ameitekeleza kwa kuagiza 20% fedha za UVIKO-19 ziende kwenye miradi ya maji.Mhe Komanya amewataka wananchi wote kulinda miundo mbinu na vyanzo vya maji

Wakizungumza, Wakuu wa Wilaya ya Maswa, Itilima na Busega waliishukuru RUWASA kwa huduma ya maji inayopatikana katika halmashauri zao, na kueleza kuwa kuna baadhi ya maeneo upatikanaji wa maji ni wa 65% tu, na hivyo ni matumaini yao kuwa kwa usainishaji huu wa mikataba 24 ya maji kati ya RUWASA na Wakandarasi pamoja RUWASA na Local Fundi,upatikanaji wa maji utaongezeka na utekelezaji wa miradi hiyo utafanyika kwa mujibu wa ratiba, huku wakizingatia ubora, kwani kiasi cha fedha zilizoelekezwa kwenye miradi hiyo si ndogo.Wakuu wa Wilaya hizo waliwahakikishia wakandarasi na Local Fundi kuwa wako pamoja nao na kuwahakikishia ushirikiano wao.Mwisho

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa