• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wafugaji Simiyu Kuboresha Ufugaji Kupitia Uhimilishaji

Posted on: October 11th, 2018

Wafugaji Mkoani Simiyu wanatarajia kuboresha ufugaji wao kupitia Mpango Mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya  uhimilishaji kwa lengo la kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya mifugo, mpango unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Desemba, 2018.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha Wadau wa Mifugo mkoani Simiyu, kilichofanyika Oktoba 10, 2018 mjini Bariadi, kwa lengo la kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha  mifugo  kwa njia ya Uhimilishaji (Artificial Insermination),chini ya Uenyekiti wa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa Mpango wa Uhimilishaji  kutoka Shirika la Land O’ Lakes, Bw. Joachim Balakana amesema  shirika hilo kwa kushirikiana na mkoa wa Simiyu limelenga kuhakikisha wafugaji wa ng’ombe wa kienyeji na kisasa wanafanya uhimilishaji ili kuboresha mbari za ng’ombe wao na kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa na nyama.

“Uhimilishaji utafanyika kwa kutumia mbegu bora zilizozalishwa hapa nchini katika kituo cha Uhimilishaji Arusha, baada ya ng’ombe wa kienyeji kuhimilishwa tunategemea kupata ng’ombe chotara wa waziwa ambao watakuwa wakitoa maziwa mengi na wa nyama watakaofikia uzito mkubwa ndani ya muda mfupi”alisema Balakana.

Ameongeza kuwa kupitia mpango huu ng’ombe zaidi ya 12,000 wanatarajiwa kuhimilishwa mkoani Simiyu kuanzia Desemba, 2018, huku akibanisha kuwa kutokana na mwitikio mkubwa wa wafugaji na viongozi mkoani humo, ng’ombe zaidi ya hao waliolengwa wanaweza kuhimilishwa na ndani ya muda mfupi matokeo makubwa yakaonekana.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo una ng’ombe wengi hivyo, uhimilishaji utasaidia kuongeza thamani ya mifugo kwa upatikanaji wa mbegu bora, ambapo ng’ombe wa nyama watakuwa na uzito mkubwa wakiwa na umri mdogo, ngombe wa maziwa kutoa maziwa mengi na ngozi bora pia itapatikana.

Ameongeza kuwa mkoa huo umejipanga kuboresha ufugaji na kuwasaidia wafugaji kuona thamani ya ufugaji, huku akibainisha kuwa upo uhakika wa kuyaongezea thamani mazao ya mifugo hususani maziwa, kutokana na uwepo wa kiwanda cha maziwa wilayani Meatu ambacho kiko katika mpango wa  kupanuliwa ili kukiongezea uwezo katika uzalishaji.

Akiwasilisha taarifa ya hali ya uboreshaji  mifugo ya mkoa wa Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Gamitwe Mahaza amesema jumla ya ng’ombe 348 waliozaliwa kwa njia ya uhimilishaji kati ya ng’ombe 1,598,935 waliopo, hivyo mkoa unaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhimiza uhimilishaji katika halmashauri zote mkoani humo.

Dkt. Gamitwe ametaja moja ya juhudi hizo kuwa ni pamoja na kuzielekeza Halmashauri kutenga asilimia 15 ya mapato ya ndani yatokanayo na mifugo kwa lengo la kuanzisha mfuko wa maendeleo wa mifugo, kuzihamasisha halmashauri kununua vifaa vya uhimilishaji na kununua madume bora.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa wafugaji na wafugaji wamesema wameupongeza uongozi wa mkoa kwa kufikiri namna ya kuboresha ufugaji kupitia na mpango wa uhimilishaji na wakaeleza kuwa wameupokea mpango huo na kuomba uanze kutekelezwa mara moja ili waweze kuona tija katika ufugaji wao.

“Naishukuru Serikali kuleta mpango huu wa kuhimilisha ng’ombe wetu nimeupokea kwa furaha sana na ninaomba wataalam waje haraka kutuelimisha wafugaji, ili uanze kutekelezwa haraka tupate kuona  faida ya ufugaji, tupate maziwa mengi na ng’ombe wa nyama wenye uzito mkuwa kama mtaalam alivyotueleza” alisema Bw. Mathias Gabriel  Mfugaji kutoka Kijiji cha Mwanegele wilayani Maswa.

“ Nimeupenda mpango wa uhimilishaji ambao utasaidia kuboresha ng’ombe wa kienyeji tulionao sasa, na mimi kama Katibu wa Wafugaji Itilima napendekeza mpango huu utakapoanza uanzie kwangu, ili wafugaji wengine waje wajifunze kutoka kwangu”  Katibu wa Wafugaji Wilaya ya Itilima, Samson Kingi Guma alieleza.

Mpango mkakati wa uboreshaji wa mifugo kwa njia ya Uhimilishaji Mkoani Simiyu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo,  Shirika la Land O’ Lakes chini ya Mradi wa Ushirikishwaji wa Sekta ya Umma na binafsi katika utoaji wa huduma za Uhimilishaji (PAID), kwa ufadhili wa Mfuko wa wakfu wa Bill na Melinda Gates.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/10/wafugaji-simiyu-kuboresha-ufugaji.html


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa