• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wafugaji Nyuki watakiwa Kuanzisha Viwanda Vidogo Kuongeza Thamani Mazao ya Nyuki

Posted on: October 4th, 2017

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani  amesema Wafugaji Nyuki wanayo fursa kubwa ya kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuchakata, kufungasha na kuongeza thamani mazao ya nyuki na kutengeneza vipodozi kutokana na mazao ya nyuki.

Mhandisi Makani  ameyasema hayo jana wakati alipozungumza na wafugaji wa nyuki na wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, chini ya Kauli Mbiu “UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA UNACHANGIA KATIKA UKUAJI WA VIWANDA”

Amesema Mazao ya Nyuki ni malighafi ya Viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya vyakula vinavyotumia asali, viwanda vya dawa na vipodozi na viwanda vya utengenezaji vinavyotumia nta katika kuzalisha maturubai, dawa za kung’arisha viatu na bidhaa nyingine, hivyo wafugaji  wanao wajibu wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki na ujuzi wa kuyaweka katika ubora na kuyaongezea thamani.

Aidha, ametoa wito kwa wafugaji wa nyuki kuungana katika vikundi vyenye usajili ili waweze kuzalisha asali kwa wingi na yenye kufanana, kwa kuwa ikiwa watazalisha kila mmoja kwa utaratibu wake, asali hiyo haiwezi kuchanganywa na itakuwa na ubora na sifa tofauti, lakini ikiwa wataungana na kuzalisha asali nyingi kwa pamoja wakaipima kwa viwango vya ubora unaotakiwa wataweza kupata soko.

Sanjali na hilo amesema Serikali itahakikisha inawaunganisha wafugaji nyuki na walaji wa ndani na nje na akabainisha kuwa kwa miaka zaidi ya 11 imekuwa na ushirikiano na soko la Ulaya ambapo sampuli za asali kutoka maeneo mbalimbali zimepelekwa Ulaya na taarifa za maabara zinathibitisha kuwa asali ya Tanzania ni salama kwa afya ya mlaji.

Aidha, amesema katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki Serikali pia inaendelea kutoa elimu kwa wafugaji wa nyuki  kuachana na matumizi ya mizinga ya asili ambayo ni duni na inachukua nafasi kubwa wakati uzalishaji wake ni mdogo na kuwahamasisha kuanza kutumia mizinga ya kisasa.

“ Nawaagiza Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki nchini na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia jukwaa hili, kwamba mbuni njia rafiki ya kuweka msisitizo katika utoaji wa elimu, uhamasishaji na kupima mafanikio kila mwaka; taarifa ya utekelezaji wa maagizo haya itolewe mara kwa mara, taarifa ya kwanza baada ya agizo hili itolewe katika siku ya maadhimisho kama haya mwaka kesho 2018” aliagiza Naibu Waziri

Katika hatua nyingine Mhe. Makani amepongeza juhudi zinazofanywa na Mradi wa LVEMP II katika kuboresha mazingira na kubainisha kuwa pamoja na kuhifadhi rasilimali za asili za Bonde la Ziwa Victoria ambayo husaidia kutunza vyanzo vya maji  na mazingira hayo yanafanywa kuwa mazingira bora kwa ufugaji nyuki, ambapo katika wilaya ya Itilima kuna vikundi 22 vyenye mizinga 2080 ya nyuki vinavyofadhiliwa na LVEMP.

Akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki amesema idadi ya wafugaji na mizinga ya nyuki imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo kwa sasa kuna jumla ya vikundi 91 vyenye jumla ya mizinga 5824 na akaahidi kuwa mkoa utaendelea kusimamia uboreshaji wa mazingira ya ufugaji nyuki na kusimamia vikundi vinavyoanzishwa katika Halmashauri., ili wafugaji wanufaike na kujiimarisha kiuchumi

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Ndg.Herberth Haule amesema shughuli ya ufugaji wa nyuki  inasaidia katika uhifadhi wa mazingira na  kujenga uchumi kwa wananchi hususani vikundi vinavyojishughulisha na kazi hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Ezekiel Mwakalukwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za Afrika zinazoruhusiwa kuuza asali yake katika soko la Ulaya na nchi ya China

Nao wafugaji wa nyuki na wajasiriamali wa mazao ya nyuki wameiomba Serikali pamoja na wadau wengine kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza vifungashio kwa kuwa suala hilo ni changamoto kwao ambayo  inawalazimu kuagiza vifungashio nje ya nchi kwa kutumia gharama kubwa.

Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa kwa mwaka 2017 yameadhimishwa kwa mara kwanza Mkoani Simiyu yakiwa ni maadhimisho ya tano kufanyika hapa nchini, ambapo kwa mara ya kwanza  yalifanyika mwaka 2013 Mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) (kulia) kabla ya kuanza safari kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani humo.

Kutoka kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt. Titus Kamani, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi wakizungumza jambo,   wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) (mwenye skafu) akiangalia mazao ya Nyuki alipotembelea Banda la maonesho la Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wilayani Itilima, wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika  Mkoa Simiyu.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa