• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wadau watoa msaada wa Fedha, Chakula kuwezesha Kambi ya Kitaaluma kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita Simiyu

Posted on: April 8th, 2018

Wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu wametoa shilingi Milioni 10 na Kilo 1200 za mchele , mafuta ya kula, sabuni na mahitaji mengine kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi wa kidato cha Sita walioweka Kambi ya kitaaluma wilayani Maswa kwa ajili ya kujiandaa na Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Mei.

Akizungumza wakati wa makabidhiano katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataja wadau hao kuwa ni Ofisi yake iliyotoa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuongezea posho ya walimu mahiri 40 wanaowafundisha wanafunzi hao pamoja na kununua mahitaji maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa kike.

Amesema wadau wengine ni Mbunge wa Itilima Mhe.Njalu Silanga aliyetoa kilo 500 za mchele, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kilo 300, Mkurugenzi wa Itilima kilo 100 za mchele, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi kilo 100 za mchele, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi kilo 100 za mchele na Mkurugenzi Busega kilo 100 za mchele.

Aidha, amesema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imeahidi kuchangia ng’ombe wawili na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu imeahidi kuchangia kilo 100 za mchele.

Mtaka amewashukuru wadau wote walioguswa kuwachangia wanafunzi hao wa kidato cha sita  na akatoa wito kwa wazazi, viongozi na watu kutoka makundi mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Idara ya Elimu katika kuwasaidia wanafunzi hao, ili waweze kujiandaa na kufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa mwezi Mei.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa mwaka huu mkoa wetu unaingia kwenye mikoa itakayofanya vizuri zaidi Kitaifa, niendelee kuwaomba wanafunzi mliopo hapa mzingatie masomo siku 10 mtakazokaa hapa ziwe na manufaa kwenu na ninyi walimu 40 wafundisheni watoto kwa vipaji vyote mlivyojaliwa na Mwenyezi Mungu ili wafanye vizuri kwenye mtihani wao wa mwisho” alisema Mtaka.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amesema baada ya kambi hiyo ya kitaaluma kumalizika ndani ya hizo siku10 ufanyike mtihani ili kuwapima wanafunzi na akaahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni tano kwa walimu wataotunga maswali yatakayofanana na yale yatakayokuwepo katika Mtihani wa Taifa kwenye masomo yao.

Akizungumza kwa niaba ya walimu mahiri 40 wanaowafundisha wanafunzi kambini hapo Mwalimu Makame S. Makame kutoka Shule ya Sekondari Bariadi,  amesema kwa namna walivyojitolea kuwafundisha wanafunzi hao wana imani kubwa kuwa mwaka 2018 utakuwa mwaka matokeo mazuri(Kidato cha Sita)  ya kihistoria kwa Mkoa wa Simiyu.

Mwanafunzi Martina Simba kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na wadau wengine wote kwa misaada waliyoitoa na kusisitiza kuwa, kukaa kwao kambini hapo siku kumi hakutakuwa bure bali ni mwanzo mzuri wa safari yao ya mafanikio ya kuwafikisha katika mikoa itakayofanya vizuri zaidi katika Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2018.

 Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita Mkoani Simiyu ilifunguliwa rasmi Aprili 3 ikiwa na jumla ya wanafunzi1003 kutoka shule 11 na walimu mahiri 40 kwa ajili ya kuwafundisha na inatarajiwa kufungwa Aprili 13, 2018.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/04/wadau-wawachangia-fedha-vyakula.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa