• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wadau wa Pamba Mkoani Simiyu wakutana Kujadili Mstakabali wa Zao hilo

Posted on: September 6th, 2017

Wadau wa zao la pamba mkoani Simiyu wamekutana na kufanya kikao lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mstakabali wa zao hilo kuelekea katika kipindi cha msimu wa kilimo kwa mwaka 2017/2018.

Kikao hicho kimewahusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Kilimo, Wamiliki na wataalam wa Makampuni ya Ununuzi wa Pamba kutoka ndani ya nje ya Mkoa wa Simiyu ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema Mkoa huo unazalisha zaidi ya asilimia 55 ya pamba yote hapa nchini, hivyo akawataka wadau wa pamba mkoani humo kutumia vema kikao hicho kujadili kwa umakini masuala muhimu katika sekta ya pamba ili wananchi waweze kuzalisha kwa tija na kunufaika na zao hilo.

 

 Katika kikao hicho Wadau wa zao la pamba wamekubaliana kuwa kilimo cha mkataba kwa wakulima kiwe cha hiari sio lazima na elimu indelee kutolewa kwa wakulima na wanunuzi wa pamba kuona namna wanavyoweza kutumia kilimo cha mkataba kuongeza tija katika uzalishaji kwa wakulima watakao kuwa tayari.

Akichangia hoja katika kikao hicho Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Martha Zongo, amesema kilimo mkataba kikifanyika kwa makubaliano yatakayowekwa baina ya wakulima walio tayari  na makampuni yanayonunua pamba, wakulima wasio na uwezo watapata pembejeo na huduma za ugani kutoka kwa wataalam wa Makampuni hayo na kuongeza uzalishaji maana katika baadhi ya maeneo kuna upungufu wa maafisa Ugani.

Kuhusu suala la matumizi ya mbegu wadau walikubaliana kuwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu watapata mbegu zenye manyoya na zisizo na manyoya kama ilivyoelezwa na Bodi ya Pamba na ni hiari yao kuchagua mbegu watakayoitaka, hivyo elimu iendelee kutolewa kwa wakulima juu ya matumizi ya mbegu hizo ili waelewe mbegu iliyo bora zaidi kwa uzalishaji wenye tija.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza amependekeza Taasisi ya Ukaguzi na Uthibitisho wa Mbegu Nchini(TOSCI) waone umuhimu wa kufungua tawi Kanda ya Ziwa ili kufuatilia kwa ukaribu udhibiti wa mbegu za pamba na Wakala wa Mbegu (ASA) watafute mashamba pia katikakanda hii ili waweze kuzalisha mbegu kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa mbegu bora za pamba.

Vile vile katika suala la mbegu Bw. Stephen Lawrence kutoka Kampuni ya Nyanza Cotton  inayojishughulisha na ununuzi wa Pamba akiungwa mkono na wadau wengine, aliomba Serikali itoe ruzuku kwa wakulima ili waweze kumudu gharama za ununuzi wa mbegu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliwahakikishia wajumbe kuwa mapendekezo na maazimio yaliyotolewa katika kikao hicho atayawasilisha katika Kikao cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kasim Majaliwa na Wakuu wa Mikoa inayolima pamba hapa nchini kitakachofanyika Mjini Dodoma, tarehe 08/09/2017.

Baadhi ya wadau wa zao la pambaMkoani Simiyu wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili suala la Kilimo cha Pamba mkoani hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.

Mbunge wa Jimbo la Bariadi na Mmiliki wa Kiwanda cha pamba(Ginner), Mhe.Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa  pamba Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa kilimo cha  zao hilo mkoani humo.

Bi.Suzan Mollel kutoka katika Kampuni ya OLAM inayojishughulisha na ununuzi wa pamba iliyoko wilayani Bunda, akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa