• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wachungaji, Waganga wa Jadi wacheza mpira Kulenga Kupinga Mauaji ya Wenye Ualbino

Posted on: May 31st, 2017

Mkoa wa Simiyu umeweka historia ya Mchezo wa Mpira wa Miguu baina ya wachungaji na waganga wa jadi ikiwa ni makubaliano ya kutoa ujumbe wa kupinga mauaji ya watu wenye Ualbino na vikongwe kwa kupiga maarufuku Ramli Chonganishi ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa mauaji hayo.

Mchezo huo kati ya wachungaji na waganga wa jadi umefanyika  siku moja kabla ya kufanyika burudani kubwa ya utamaduni wa asili almaarufu Mbina ambayo hufanyika kila mwaka Mei 31,baada ya wakulima kumaliza msimu wa kilimo .

Pande zote mbili kwa  pamoja zilikubaliana  kuwa utaratibu wa kufanya vikao na michezo utakuwa endelevu na utafanyika kila mwaka kwa kuzunguka katika wilaya zote ili kuhakikisha mauji ya watu wenye ualbino na vikongwe yanakomeshwa kabisa.

Askofu wa K.K.K.T Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt.Emmanuel Makala amesema Kanisa liko tayari kukemea kwa wazi mauaji ya watu wenye ualbino na linaunga mkono juhudi za Serikali za kulinda amani na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Naye Mtemi Charles Balele Doto ambaye ni Katibu wa Umoja wa Watemi Kabila la Wasukuma amesema waganga wa jadi kazi yao ni kutoa huduma za tiba asili kwa watu na siyo kufanya ramli chonganishi zinazopelekea mauji ya watu wenye ualbino, akawataka wanaofanya hivyo waache mara moja kwa kuwa ni wababaishaji na wanadhallisha ya huduma ya tiba asili.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kukamilika,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amewapongeza kwa uamuzi huo ambao unatoa Taswira mpya kwa mkoa wa Simiyu wa kuondokana na dhana iliyokuwepo ya mauaji na kuwa mkoa wa kimaendeleo na kuagiza michezo mbalimbali kufanyika kila mwezi ili kuendeleza vipaji vya mbalimbali vya wanamichezo.

Aidha, amesema Mkoa huo una agenda ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja ama ununue au ukodishe Simiyu, Watanzania Tupende vya kwetu”hivyo akawataka wananchi kuchangamkia fursa hizo kwa maendeleo yao na kuachana na imani potofu kuwa Viungo vya Mtu mwenye ualbino vitawapa utajiri.

“Simiyu tunajenga viwanda utajiri wako wewe usiue albino utajiri wako lima pamba uuze kwenye kiwanda cha nguo, jiandae kuwa wakala, soma vizuri uwe mfanyakazi, jiandae kuzalisha malighafi ya Viwanda vya Rais wetu Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli”  alisema.

“Tarehe 09 Mwezi Juni tunapokea hundi ya shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha chaki Maswa, Tarehe 12 Juni tunaanza upembuzi yakinifu wa viwanda vyetu viwili; upanuzi wa kiwanda cha maziwa Meatu na kiwanda cha kusindika nyanya na pilipili ili tutengeneze tomato sauce na chili sauce. Bariadi tutajenga kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba, Itilima tutajenga kiwanda cha kutengeneza sabuni zote hizi ni fursa” alisema

Mtaka ameongeza kuwa wazazi wote walio na watoto wenye ulemavu wa aina yoyote wasiwafiche wawatoe kwa Serikali imewatengenezea mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kulinda haki zao.

Wakati huo huo amewataka wananchi kuvitumia vituo vya kutolea huduma za Afya kwanza kila wanapohitaji matibabu badala ya kukimbilia kwa Waganga wa jadi hali inayopelekea wengi wao kuchelewa kupata  huduma wanapoteza maisha na kuingia katika ramli chonganishi kwa kuamini kuwa wamerogwa.

Katika Mtanange huo uliofanyika katika uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi Waganga wa kienyeji walikubali kichapo cha Magoli mawili kwa nunge(sifuri) kutoka kwa watumishi wa Mungu(Wachungaji).

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa