Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wamekutana na Wabunge wa Mkoa huo mjini Dodoma katikakikao maalum kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumiwa Viwanda Mkoani Simiyu.
Pamoja na kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau hao kuhusu Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu, kikao hicho piakilikusudia kupata baraka za Wabunge wa Mkoa huo juu ya miradi ya uanzishwajiwa Viwanda katika Halmashauri zote sita.
Katika kikao hiki wajumbe wamepata fursa ya kupitia maandiko ya miradi ya uanzishwaji wa viwanda yaliyowasilishwa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote sita; viwanda ambavyo vitajengwa katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Simiyu chini ya utekelezaji wa Kauli Mbiu ya "Wilaya Moja Bidhaa Moja".
Miradi iliyowasilishwa ni pamoja na upanuzi waKiwanda cha kutengeneza Chaki wilayani Maswa, Upanuzi wa kiwanda cha kusindikamaziwa wilayani Meatu ambapo kiwanda hicho kitaongeza uzalishaji wamaziwa yakiwemo maziwa ya unga.
Miradi mingine ni ujenzi wa kiwanda chakutengeneza vifungashio wilayani Maswa,kiwanda cha kutengeneza sabuni zamaji,miche na za unga wilayani Itilima, kiwanda cha kutengeneza Tomato sauce naChill sauce Busega, kiwanda cha kusaga nafaka na kupaki unga katika Halmashauriya Mji wa Bariadi na kiwanda cha kuchakata ngozi na bidhaa za ngozi katikaHalmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Wabunge wa Mkoa wa Simiyu chini ya Uenyekitiwa Mbunge wa Bariadi,Mhe.Andrew Chenge kwa pamoja wamepongeza juhudizinazofanywa na viongozi na watendaji mkoani humo na kuunga mkono miradi yoteya uanzishwaji wa Viwanda , ambapo hatua inayofuata sasa ni kufanyika kwaUpembuzi Yakinifu kwa miradi hiyo na kuanza utekelezaji.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa waSimiyu Mhe Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuhakikishaazma ya Serikali ya awamu ya tano ya Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda inatekelezwa kwa vitendo.
Naye Katibu Tawala Mkoa,Ndg Jumanne Saginiamesema Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii ya (ESRF)wataanza kufanya upembuzi yakinifu wa mradi wa upanuzi wa kiwanda chakutengeneza chaki na watakamilisha katika kipindi cha wiki wiki mbili, wakatiupembuzi yakinifu kwa miradi mingine utafanywa na kukamilika katika kipindicha miezi miwili.
Kikao hiki kimehusisha baadhi ya wajumbe yaKamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,Wabunge wa Mkoa huo, Wakurugenzi wa Halmashauri,Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Mipango na Wanasheria waHalmashauri zote za mkoa huo,wataalam wa masuala ya Viwanda pamoja na wadauwengine wa Uwekezaji kutoka NSSF.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa