• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Viongozi wa Dini, Siasa na Kimila Washirikishwe Kuelimisha Jamii Kuzuia Vifo Vitokanavo na Uzazi-RC Mtaka

Posted on: May 3rd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa Serikali mkoani hapa kuona umuhimu wa kuwashirikisha viongozi wa dini, siasa na wa kimila katika utoaji wa elimu kwa jamii na kuwahamasisha wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi..

Mtaka ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama uliofanyika Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.

“ Ni vizuri tukaongeza wigo wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa mama wajawazito kuhudhuria kliniki kipindi cha ujauzito na kuhakiksha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya; viongozi wa dini,siasa na wa kimila wana nafasi kubwa kwenye jambo hili muone namna ya kuwashirikisha “ alisema Mtaka.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) imeboresha vituo vya kutolea huduma, hivyo ni vema jamii ikaelimishwa umuhimu wa kutumia huduma za afya ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Katika hatua nyingine Mtaka ameishukuru UNFPA kwa namna ilivyosaidia katika ujenzi wa miundombinu ya afya,vifaa na vitendea kazi kama magari ya kubeba wagonjwa huku akisisitiza viongozi na watendaji walioshiriki katika uzinduzi wa kampeni hii kutoka na dhamira ya kuwavusha salama akina mama wajawazito na watoto na kupinga vifo vitokanavyo na uzazi..

Mwakilishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dinna Atinda ameusisitiza uongozi wa mkoa kusimamia vituo vinavyotoa huduma za afya za msingi na dharura kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa wananchi.

Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Salome Mwijuma ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwasaidia wanawake wajawazito waweze kuhudhuria kliniki muda wote, wapate lishe bora na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ili wajifungue salama.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Mageda Kihulya amesema mwaka 2015 watoto 680 walifariki na mwaka 2018 watoto 640 walifariki, wakati kwa upande wa akina mama wanaojifungua vifo vimepungua kutoka 48 mwaka 2015 na kufikia 40 mwaka 2018, jambo ambalo linaonesha kuwa nguvu ya ziada kutoka wadau mbalimbali inahitajika kumaliza tatizo hili.

Dkt. Mageda amesema sababu zinazosababisha vifo vingi vya akina mama wajawazito kama vile kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua na mkingamo wa uzazi zinaweza kuzuilika, hivyo akatoa wito kwa wakina mama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma kuzuia vifo hivyo, huku akisisitiza watoto chini ya miaka mitano nao wapewe chanjo kuzuia vifo..

Makamu Mwakilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, Dkt. Hashina Begum amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika jitihada mbalimbali za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/viongozi-wa-dini-siasa-na-kimila.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa