• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Viongozi Simiyu Waaswa Kutumia Busara Badala ya Nguvu

Posted on: March 14th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Viongozi wa Serikali mkoani hapa kutumia busara na akili badala ya kutumia nguvu katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo waliyopo na kuhakikisha ufumbuzi unaotolewa unaleta tija kwa wananchi.

Mtaka ametoa rai hiyo wakati akifungua  kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.

“Wito wangu kwa viongozi wenzangu tupunguze kutumia nguvu, tuongeze matumizi ya akili tuone matokeo kwa wananchi wetu, leo tunapitisha mapendekezo ya bajeti ya mkoa mwaka 2021/2022 lakini ningetamani kuona miradi mipya ya Halmashauri inayogusa watu, halmashauri zetu zijielekeze kwenye kuanzisha miradi ambayo itakuwa vyanzo vipya vya mapato,” alisema.

Aidha, Mtaka ametoa rai kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri kupima tija ya vikao vyao na kuhakikisha vikao wanavyokaa vinaleta tija ikiwa ni pamoja na namna vikao hivyo vinavyosaidia kubuni na kuongeza vyanzo vya mapato.

Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti ya Mkoa wa Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi-Sehemu ya Mipango na Uratibu, Bw. Donatus Weginah amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Simiyu inatarajiwa kutengewa shilingi bilioni 200.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, mishahara na matumizi mengineyo.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge  Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa ameunga mkono mapendekezo ya mpango na bajeti ya mkoa na kuahidi ushirikiaono wa wabunge hao katika kupitisha bajeti hiyo bungeni.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa kwa viongozi wote mkoani Simiyu kushirikiana na vyombo vinavyohusika na usimamizi wa fedha kudhibiti na kusimamia matumizi ya fedha zote za Serikali ili ziweze kuleta tija.

Akitoa salamu kwa naiba ya Chama cha Mapinduzi, Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba amewashauri wataalam kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kubuni vyanzo na mbinu za kuongeza mapato kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mkoa wa Simiyu .

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2021/03/viongozi-simiyu-waaswa-kutumia-busara.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa