• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Uongozi wa Mkoa Simiyu Wabaini Ubadhilifu wa Shilingi Milioni 55 Busega

Posted on: September 25th, 2019

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umebaini Ubadhilifu wa kiasi cha shilingi 55,580,000/= ambazo ni sehemu ya mkopo uliotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urasimishaji wa makazi Viwanja 3700 katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Busega uliofanywa na Watumishi wanne wa Halmashauri hiyo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakati akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya  fedha za mradi huo katika kikao cha  Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 Busega Septemba 06,2019 Nyashimo Busega.

Sagini amewataja watumishi waliohusika katika ubadhilifu huo kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri, Anderson Njiginya, Mkuu wa Idara ya Ardhi, Magesa Magesa, msimamizi wa mradi Raymond Mahendeka na mhasibu wa mradi,Augustina Kitau na kuwataka kurejesha fedha hizo mara moja na kushauri mamlaka zao za nidhamu kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria

Sagini ameongeza kuwa timu ya uchunguzi imebaini mapungufu mbalimbali katika matumizi ya fedha hizo ikiwa ni pamoja na ukikwaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha, ukiukwaji wa masharti ya mkataba, ukiukwaji wa sheria kanuni na taratibu za manunuzi ya Umma, udanganyifu na uzembe na usimamizi dhaifu wa Mradi.

“Kutokana na mapungufu yaliyobainishwa katika uchunguzi huu Uongozi wa mkoa unaelekeza watumishi waliohusika warejeshe fedha hizo haraka ili mradi utekelezwe kama ilivyokusudiwa na tunashauri mamlaka za nidhamu zichukue hatua stahiki kwa watumishi hao kwa mujibu wa sheria na taratibu za Utumishi wa Umma,” alisema Sagini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti amewashukuru viongozi wa Mkoa kutuma wataalam wa Mkoa kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi na kumuagiza Mkurugenzi kuanzisha utaratibu wa kuwachukulia hatua watumishi waliohusika walio chini  ya mamlaka yake kama  viongozi wa mkoa walivyoelekeza.

Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe, Goodluck Nkalango amesema madiwani wa Halmashauri ya Busega wakiwemo wajumbe wa kamati inayoshughulikia masuala ya ardhi hawakushirikishwa katika utekelelezaji wa mradi wa urasimishaji, makazi jambo ambalo lilipelekea wananchi kutokuwa na taarifa sahihi za mradi ikiwemo utaratibu wa kuchangia gharama za upimaji.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Alex Mpemba amesema TAKUKURU imepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi na itaanza kuifanyia kazi mara moja kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai kwa waliohusika.

“Tumeipokea taarifa ya uchunguzi kupitia kikao cha baraza la dharura na kwa sababu wenzetu wa ukaguzi wamemaliza kazi yao na sisi tutaanzia pale walipoishia kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai,” alisema Mpemba.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega ilipokea mkopo wa shilingi 100,000,000/=kutoka Wizara ya Ardhi kutekeleza Mradi wa urasimishaji wa makazi viwanja 3700 katika kata za Mwamanyili, Mkula, Kiloleli na Lamadi; kwa mujibu wa taarifa ya Uchunguzi hadi kufikia Septemba  06, 2019 utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimi 8.5 na fedha zilizokuwa zimetumika ni  asilimia 98.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/09/uongozi-wa-mkoa-simiyu-wabaini.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa