• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Chuo cha VETA Mkoa wa Simiyu Kuanza Kujengwa Mwezi Machi, 2018

Posted on: December 27th, 2017

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako amesema Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) cha Mkoa wa Simiyu kuanzia mwezi Machi, 2018.

Waziri Ndalichako ameyasema  hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani humo.

“Kesho tarehe 28/12/2017 kwenye magazeti kutatoka tangazo la zabuni ya ujenzi wa VETA ya Mkoa wa Simiyu na tunategemea kujenga VETA ya Kisasa itakayohudumia Mkoa na inayoendana na mahitaji ya sasa; tukitangaza zabuni kesho itachukua siku 30 kupokea zabuni unahitajika mwezi mmoja kufanya tathmini, nawaahidi kuwa ujenzi utaanza mwezi Machi” alifafanua Profesa Ndalichako.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inasisitiza juu ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda inatambua umuhimu wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi ndiyo maana imejipanga kujenga vyuo hivyo pamoja na kuimarisha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.

Aidha, Profesa Ndalichako amepongeza ongezeko la wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza na akasisitiza kuwa Wizara ya Elimu ambayo ndiyo inayotunga Sera itahakikisha inasimamia kikamilifu ili  wanafunzi wote wanaoanza darasa la kwanza wamalize masoma yao.

Amesema ongezeko hilo ambalo limesababishwa na mwamko chanya wa wazazi baada ya kuanza kutekelezwa kwa  mpango wa elimu bila malipo limepelekea upungufu wa miundombinu shule na ndiyo maana Serikali kuu inashirikiana na Halmashauri pamoja na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ili kukabiliana na upungufu kupitia Mradi wa Lipa kulingana na Matokeo(P4R).

“Kupitia mradi wa Lipa kulingana na Matokeo tumeshajenga jumla ya vyumba vya madarasa 1104, matundu ya vyoo 3396, mabweni 261. Tunaendelea pia kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu kwa ujumla, kwa maana ya ukarabati katika vyuo vya Ualimu ambapo tumeshakarabati vyuo 17 na shule kongwe 46 kati ya shule 88 zimeshakarabatiwa” alisema Waziri.

Profesa Ndalichako amepongeza Uongozi wa Wilaya ya Itilima kwa kutumia vizuri jumla ya shilingi bilioni 2.177 za Mradi wa Lipa Kulingana na matokeo(P4R) ambazo zimetumka kujenga vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo  wilayani humo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema katika kipindi cha mwaka 2018-2020 Mkoa huo umejiwekea mpango wa kujenga mabweni kwa wanafunzi wa kike katika kila shule ili kuwaondolea adha ya kutembea mwendo mrefu na changamoto nyingine.

Akimshukuru Waziri wa Elimu kwa kupeleka fedha za Mradi wa Lipa kulingana na matokeo (P4R) katika Wilaya ya Itilima ambazo zimesaidia upatikanaji wa Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga amesema Wilaya hiyo imetekelezaji wa mradi huo kwa kufuata taratibu na miongozo yote  ya Serikali kwa kushirikiana na wananchi.

Hii ni ziara ya kwanza kwa Waziri Ndalichako Mkoani Simiyu ambayo imempa nafasi ya kutembelea, kuweka mawe ya msingi, kukagua na kufungua vyumba vya madarasa, mabweni katika maeneo tofauti Wilayani Itilima ikiwemo Kijiji cha Habiya, Lagangabilili, Itilima, Mahembe na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Luguru.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi (kulia) wakati akikagua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Lagangabili, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo(P4R) katika Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani Itilima


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako akipokelewa na viongozi wa Wilaya ya Itilima mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja.

Vijana wa Skauti wilaya ya Itilima wakivisha Skafu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(mbele kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya itilimana Mkoa wa Simiyu mara baada ya kukagua jengo la Bweni linalojengwa kwa ya wanafunzi wa kidato cha Tano na sita watakapoanza kusoma shuleni hapo



Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa