Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Agosti 8, 2019 ,anatarajiwa kuzindua kanzi data ya usajili wa wakulima kupitia mazao nane ya kimkakati, itakayosaidia kujua idadi ya wakulima sambamba na wakulima kujua takwimu za mazao na upatikanaji wa masoko kwa urahisi kupitia njia ya mtandao .
Mhe. Hasunga ameyasema hayo Julai 30, 2019 wkati akikagua maendeleo ya maandalizi ya maonesho ya Nanenane Kitaifa Mkoani Simiyu, ambapo amesema pamoja na kuzindua kanzi data ya wakulima Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa pia kuzindua mfumo wa kielectroniki utakaosaidia kujua idadi ya wakulima, mahali walipo,mazao wanayolima na ukubwa wa maeneo wanayolima.
“Tunataka kili Mtanzania popote alipo akitaka takwimu sahihi awe anaweza kuingia kwenye mfumo na akaziona, ukitaka wakulima wa pamba wa pamba waonekane, tukakitaka wakulima wa mkonge waonekane, tunataka tuwe na uwezo wa kuwaona wakulima wakubwa, wa kati na wadogo na mahali walipo” alisema Mhe. Hasunga.
Pamoja na hayo ameongeza kuwa tarehe hiyo pia Rais Dkt Magufuli atafungua soko la bidhaa ambalo litawawezesha wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi ambayo itasaidia kupata uhakika wa bei na kuepuka madalali na kuleta uwazi ili kila mkulima /mdau yoyote aweze kuona na kujua bei sambamba na kufahamiana .
Waziri Hasunga amesema kwa upande wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan , wakati akizindua maonesho ya nane nane Agosti Mosi, 2019, anatarajiwa kuzungumzia masuala ya mazinigira ambapo atazindua mkakati wa kuthibiti upotevu wa mazao utakao wezesha kujua hasara anazozipata mkulima hatua itakayopelekea kukabiliana nazo kwa wakati.
Aidha waziri Hasunga ameongeza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa atazindua bima ya mazao ambayo itasaidia kukabiliana na vihatarishi vya mazao mfano ukame na mafuriko sambamba na kuona maendeleo ya ushirika nchini na nafasi ya ushirika na namna ambavyo unawaunganisha wakulima ,wafugaji na wavuvi.
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amemtembelea mmoja wa wajasiriamali kutoka wilaya ya Meatu Deke Ndabuli Maige anayetengeneza mashine za kupukuchua mahindi ambapo mjasiriamali hiyo amesema kuwa alianza kutengeneza mashine hizo tangu mwaka 2014 na hadi sasa ameshatengeneza mashine 10 na tayari ameshauza mashine 7.
Pamoja na hayo ameongeza kuwa mashine hizo zinauwezo wa kupukuchua magunia 150 kwa siku huku akitumia lita saba za mafuta ya kuendeshea mashine hiyo kwa siku.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:- https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/tunatarajia-rais-magufuli-atazindua.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa