• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Tumieni Wakandarasi na Watoa Huduma Kutoka Simiyu- RC Kafulila

Posted on: February 16th, 2022

Mhe. Kafulila ameyasema hayo hivi karibuni  akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na mkuu wa Wilaya ya Bariadi, wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Simiyu. Mhe. Kafulila ametoa maelekezo hayo mara badaa ya kuelezwa na Meneja mradi  ambaye pia ni Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya jamii Buhnamala-Bariadi,  Bw.Bazil Ngoloka  kuwa matofali ya ujenzi wa mradi huo yanasambazwa na mtoa huduma kutoka Mwanza anayejulikana kama Arm Strong Company Limited.

Akizungumzia mradi huo Bw.Ngoloka ameleza, mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA Mkoani Simiyu ulianza tarehe 26.01.2022 kwa kazi ya awali na kazi rasmi ilianza 07/02/2022 kazi ambayo inatarajiwa kukamilika mara ifikapo 30/6/2022. Mradi huu unasimamiwa na chuo cha ufundi Arusha.

Ujenzi wa chuo cha VETA Simiyu,utagharimu kiasi cha Tsh.5,150,731,187.10,ambazo zitatumika kujenja, mabweni manne , mawili yakiwa ya kike na mawili ya kiume, majengo ya idara tisa,majengo ya utawala na huduma zinginezo 7 pamoja  na nyumba za waalimu 4. “Kwa ujumla hatua ya utekelezaji hadi sasa zimefikia  hatua ya uchimbaji wa Msingi majengo kwenye kila lot na umwagaji zege kwenye baadhi ya majengo. Kiasi cha fedha zilizotumika hadi sasa  ni  Tsh. 7.89 ml.’’Amesema Ngoloka.

Pamoja na mafaniko hayo Bw. Ngoloka, ametaja kukabialina na changamoto za ubovu wa barabara hasa kipindi hiki cha mvua na ongezeko la  bei za vifaa vya ujenzi kama nondo na hivyo kupelela kurudia mchakato wa manunuzi ili kupata bei halisi ya soko.

Aidha, Mhe Kafulila aliwataka wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na mkuu wa Wilaya ya Bariadi kutoa maoni yao kuhusiana na mradi wa ujenzi huo, ambapo  Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange alisisitiza umuhimu wa kutumia vijana wa Bariadi kufanya kazi za ujenzi katika mradi huo,badala ya kutumia vijana kutoka maeneo mengine na hasa mje ya mkoa wa Simiyu,labda iwe  tu kwa fani ambazo zinahitaji utaalamu maaluum,kwani mradi huo unategemewa kuongeza ajira kwa wakazi wa Baridi.Aidha Mhe.Kapange aliahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali  kwa Meneja wa mradi huo na kuhakikisha anapata rasilimali watu katika kamati mbalimbali za ujenzi, wanakamati ambao watatokana na uwezo wao kama ilivyoelekezwa na mkuu wa Mkoa.

Wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walisistiza, suala la  Usalama wa Vifaa vya ujenzi  katika eneo la ujenzi na mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.Aidha wajumbe walikumbusha suala laupatikanaji wa Umeme ili kazi ziweze kufanyika kwa masaa 24 (usiku na Mchana) pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.

Ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo unafanyika kwa viwango na kwa wakati Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe. David Kafulila alitoa maelekezo kwa Mamlaka ya Bonde kuja kufanya uchunguzi ili kujua maji yanapatikana wapi katika eneo husika na hatimaye Meneja mradi kuhakikisha kuwa wanachimba kisima,ambacho kitatumika wakati wa mradi wa ujenzi na baada ya mradi. Vilevile Mkuu wa Mkoa aliwaagiza  TANESCO kuhakikisha kuwa kufikia ijumaa umeme uwe  unapatikana katika eneo husika. Aidha Mhe. Kafulila aliagiza  kamati za ujenzi ziangaliwe upya na Mkuu wa Wilaya  pamoja na Mkurugenzi wasaidie upatikanaji wa rasilimali watu ambao watafanya kazi katika kamati mbaliambali. Mhe. Kafulila alisistiza kuwa upatikanaji wa rasilimali watu hao uwe kulingana na uwezo na si kwa majina.

Katika hatua hiyo hiyo Mhe. Kafulila alitoa maelekezo ya kuwasimamisha kazi  watoa huduma wote wanaotoka nje ya mkoa wa Simyu, labda iwe kwa maelekezo maalum au kwa watoa huduma wanatoa huduma za moja kwa moja kutoka kiwandani kama vile kiwanda cha nondo au Sementi, kwani kwa kufanya hivyo kutaokoa muda, kutapunguza gharama, kutaongeza mauzo, kupato na  ajira kwa wananchi wa Simiyu.Mwisho.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa