Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) imetoa msaada wa taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni 6 lengo likiwa kuunga mkono maandalizi ya kambi za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne zinazotarajiwa kuanza mwenzi Agosti, 2021 mkoani Simiyu.
Akikabidhi taulo hizo meneja wa TMDA kanda ya ziwa Sofia Mziray amesema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu ambayo ni kipaumbe cha mkoa wa Simiyu huku akiwataka amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili lengo la mkoa huo ya kushika nafasi ya kwanza kitaifa.
“Tumetoa msaada huu kuunga mkono serikali ya mkoa lakini pia tumeona tuwasaidie watoto wa kike waweze kuwepo wakati wote shule, tunataka kusiwe na kisingizio chochote mtoto wa kike kushindwa kuwepo shuleni katika kipindi fulani cha mwezi, sehemu yetu tumefanya tumewaachia ninyi, wito wangu kwenu msome kwa bidii mtimize malengo ya mkoa,” alisema Mziray.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru TMDA kwa msaada huo kuku akitoa rai kwa wazazi kutowatuma wanafunzi katika minada kwa lengo la kuuza bidhaa mbalimbali badala yake kila mzazi aone umuhimu wa elimu na kuifanya elimu kuwa kipaumbele chake kwa kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo.
Aidha, Mtaka amesisitiza wazazi wenye watoto walio katika madarasa ya mitihani kuwapunguzia kazi ili waweze kupata muda mwingi wa kujisomea kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya Taifa kwa lengo la kufikia azma ya mkoa ya kushika nafasi ya kwanza katika mitihani yote ya Kitaifa.
Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema misaada inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali wakiwemo TMDA inarahisisha kazi kwa wataalamu wa elimu wanaokuwa na wanafunzi katika kambi za kitaaluma na inachangia kuongeza ari ya kusoma kwa wanafunzi na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
Hinju ameomngeza kuwa maandalizi ya kambi za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne mkoani hapo zinazotarajia kuanza Agosti, 2021 yameshaanza.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wa kike Jackline Sonda amewashukuru TMDA kwa msaada wataulo za kike na amesema wameupokea msaada huo kwa mikono miwili huku akiahidi kuwa watasoma kwa bidii kwani miongoni mwa sababu iliyokuwa ikiwafanya baadhi ya wasichana wasihudhurie kikamilifu siku zilizopangwa za kuwepo darasani tayari imepatiwa ufumbuzi.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2021/05/blog-post_8.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa