• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

TCRA yatoa Elimu kuhusu Huduma na Kuhama Mtandao Mmoja wa Simu kwenda mwingine Bila kubadili Namba

Posted on: September 26th, 2017

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP) mkoani Simiyu.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mjini Bariadi Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano Mwesigwa Felician kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA), amesema huduma hii ni ya hiari  na inampa uhuru na kumwezesha mtumiaji wa huduma ya mawasiliano kuhamia mtandao wowote anaoutaka na kuendelea kupata mawasiliano bila kulazimika kubadili namba yake ya simu.

“Namba ya simu ya Mteja itabaki ile ile na itakuwa ni kitambulisho chake, yaani (NAMBA YAKO KITAMBULISHO CHAKO) kokote atakapohamia watu watampata, hakuna haja ya kuwataarifu marafiki,familia,  wafanyakazi wenzake au washirika wenzake katika shughuli zake kama ilivyo sasa. Tunatoa elimu hii kwenu waandishi wa habari ili na ninyi muifikishe kwa wananchi kupitia kazi zenu” amesema Mhandisi Mwesigwa.

Amesema huduma hii inamwezesha mtumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua mtoa huduma mwenye huduma bora zaidi(quality of service), huduma nzuri kwa wateja(customer care services), ubunifu katika kutoa huduma zake hivyo kuongeza ushindani kwenye sekta ya mawasiliano na kuchochea utoaji huduma bora na zenye gharama nafuu.

Ameongeza kuwa huduma hii inatolewa kwa wateja wa malipo ya kabla(pre paid) na malipo baada ya huduma(post paid) kupitia vituo vya mauzo au wakala anayetambuliwa mtoa huduma (Makampuni ya Mawasiliano/Simu), ambapo watumiaji wa mawasiliano watakaohitaji huduma hiyo watatembelea maeneo hayo ili kupewa utaratibu wa kuhama.

“Mtu anayetaka kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadiliha namba yake anapaswa kufika katika Vituo vya mauzo au wakala wa mtandao anaotaka kuhamia, kupata utaratibu na akiona ipo haja ya kuhama tena itamlazimu akae kwa mtoa huduma huyo mpya kwa muda usiopungua siku 30 kabla ya kurudi kwa yule awali au kuhamia kwa mwingine” amesisitiza Mhandisi Mwesigwa.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa Bidhaa za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mamlaka ya Mawasiliano, Thadayo Ringo amesema huduma hii hapa nchini imeanza Machi Mosi mwaka huu na mpaka kufikia mwezi Juni 2017 takribani wananchi 15,000 walikuwa wameshaitumia huduma hii

Aidha, Ringo ameongeza kuwa Tanzania ni nchi ya Tisa Barani Afrika kutoa huduma hii katika mawasiliano, ambapo amebainisha nchi nyigine zinazotoa huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila kubadili namba (MNP) kuwa ni Kenya, Rwanda, Botswana, Afrika ya Kusini, Ghana, Senegal, Namibia na Misri.

Huduma hii ya kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani inatolewa kwa watumiaji ambao namba zao zinatumika yaani hazijafungiwa au kusimamishwa kwa muda.

Baadhi ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Simiyu wakisikiliza Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano Mwesigwa Felician kutoka TCRA(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutoa elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP).

Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa Bidhaa za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Thadayo Ringo akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi mkoani Simiyu wakati wa kikao kilicholenga kutoa Elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP).

Baadhi ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Simiyu wakisikiliza Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano Mwesigwa Felician kutoka TCRA(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutoa elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP).


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa