• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

TARURA,Hakikisheni Mnawapa KAzi Wakandarasi Wenye Uwezo-RC KAFULILA

Posted on: January 3rd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila ameyasema hayo leo hii, wakati wa tafrija fupi ya kusaini mikataba ya shughuli za matengenezo ya Barabara kwa fedha za tozo za mafuta, iliyoandaliwa na TARURA Mkoa wa Simiyu.

Mhe. Kafulila, ameeleza hayo wakati akishuhudia usainishaji wa mikataba ya miradi 19 ya matengenezo ya barabara yenye thamani ya Tsh.7.5 bilioni. Kati ya miradi hiyo 19, miradi 18 itatekelezwa kwa fedha za tozo za mafuta, ambazo thamani yake ni Tsh.7.1bn sawa na asilimia 95. Mhe. Kafulila amebainisha, kulingana na taarifa za wataalam wa masuala ya tozo, wataalam hao husema kuwa, ukitoza lazima uonyeshe manufaa ya hizo tozo kwa wananchi, na  leo tunajionea uhalisia kwani 95% ya fedha zinatokana na tozo zitatumika katika shughuli za matengenezo ya Barabara Mkoani Simiyu.“Hivyo ni vyema kila mkandarasi kutekeleza mkataba kwa jinsi mlivyosaini, kwani  uzoefu wa mikataba midogomidogo na baadhi ya wakandarasi ambao hawana vifaa kufanya kazi chini ya kiwango.Nielekeze Mamlaka za barabara TARURA mhakikishe mnawapa kazi wakandarasi wenye uwezo. Maana chini ya hapo sio kwamba tutavunja mkataba na huyo mkadarasi bali pia na wewe kama kiongozi, utawekwa kwenye kiulizo  yaani (black listed)” Amesema Kafulila.

Mkuu wa Mkoa amewataka Wakandarasi kuondokana na mazoea na kazi na badala yake kufanya kazi kwa wakati na weledi na kutolea mfano makandarasi wa Matongo ambaye kazi yake ipo chini ya kiwango na hivyo kumtaka Kaimu  Meneja wa TARURA, atoe maelezo ndani ya siku 3 kwanini mkandarasi huyo asifutiwe mkataba.”Sitosita kufuta mikataba yote kama mnaleta ujanja ujanja. Wakandarasi wote mnatakiwa muwe na ratiba ya utekelezaji wa kazi zenu, nikipita nipate maelezo ya kina mmefikia wapi na kwa nini.Tekelezeni mikataba yenu kwa ufanisi na viwango”Amesisitiza Mhe. Kafulila.

Wakati huo huo Mhe.Kafulila amewataka Wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa mikataba yote inayofanywa kwenye Wilaya zao , kwani hizo ni fedha za Serikali. “Mradi wowote wa Serikali unaotekelezwa kwenye Wilaya yako ni wajibu wako kujua mkandarasi ni nani, mradi unagharimu kiasi gani, utachukua muda kiasi gani, na ratiba ya utekelezaji. Hii itasaidia kujua kazi gani inafanyika lini na baada ya muda gani itakuwa imefikia wapi.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange amewataka Wakandarsi hao kutilia maanani maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na kuendana na kasi yake.

Akizungumza Kaimu Meneja TARURA- Simiyu Eng. Mathias Mgolozi , ameeleza kuwa bajeti iliyoidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa Mkoa wa Simiyu ni Tsh.18.38 bn kati ya hizo kiasi cha Tsh 5.698 bn ni fedha kwa ajili ya za matengenezo ya barabara,Tsh.4.2 bn  kutoka mfuko wa jimbo, na Tsh.8.2 bln fedha ya tozo. “kwa siku ya leo jumla ya Mikataba 19 itasainiwa. Utekelezaji wa mikataba 18 yenye thamani ya Tsh.7.1 bn itatekelezwa kutokana na  fedha ya tozo, wakati mkataba mmoja wa mradi wa daraja la Ngashanda wenye thamani ya Tsh.429,975,500/- utatekelezwa kutokana na  fedha maalum za mradi huo. Miradi yote 19 itawanufaisha wananchi wa majimbo 8 ya mkoa wa Simiyu. Mkoa wa Simiyu una Mtandao wa barabara wenye kilometa za Mraba zipatazo 4163.83.Kati ya hizo KM 1355.26 ambazo ni sawa na 33% ndizo zinazohitaji matengenezo. Matengenezo  ya KM 923.96  yanategemea fedha za ukarabati wa barabara, KM 280.6 fedha za tozo na KM 150.7 mfuko wa jimbo. Utekelezaji wa mikataba hii utaanza 17/1/2022 na kukamilika 31 Julai ,2022.

Akizungumza mwakilishi wa wakandarasi Eng. Lameck Okesh kutoka kampuni ya Nice Construction Limited amesema kuwa wapo tayari kutekeleza majukumu yako kama walivyokubalina na kuiomba Serikali kuwalipa kwa wakati. Mwisho.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa