• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

TARURA Watakiwa Kusimamia Utekelezaji wa Miradi ya Barabara kwa Weledi

Posted on: December 4th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) Mkoani humo kusimamia utekelezaji wa Miradi ya  ujenzi wa barabara na madaraja kwa kuzingatia weledi.

Mtaka ametoa wito huo wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa huo, kichofanyika leo Mjini Bariadi Mkoani humo.

" Nawaomba TARURA mfanye kazi kwa kuzingatia weledi, siyo madaraja yanajengwa mnapeleka karavati zinavunjika kabla daraja halijajengwa, mahali pa kuweka kokoto mnaweka udongo, mtaidhalilisha taaluma; ningeomba mzingatie weledi kwa sababu mkifanya vibaya wananchi watatushtaki watasema tumeanzisha wakala ambaye hana maana kwao" amesema Mtaka.

Ameongeza kuwa Uongozi wa Mkoa wa Simiyu haujapata shida juu ya miradi ya barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), hivyo ipo haja pia kwa TARURA kusimamia utekelezaji wa miradi yake katika ubora, kwa kuwa Miradi hiyo imeondolewa katika Halmashauri (Mabaraza ya Madiwani) na kupelekwa TARURA, ili ipangiwe mipango na kusimamiwa na wataalam pekee kwa lengo la kuonesha utofauti kiutendaji na umuhimu wa Wakala huo katika kuwapa huduma bora wananchi.

Wakati huo huo Mtaka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa shilingi Bilioni 86.1 kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara ya Bariadi -Maswa yenye urefu wa Kilomita 49.7 kwa kiwango cha lami, ambayo amesema ikikamilika itaifanya Bariadi na Maeneo mengine ya Mkoa huo kama Malampaka(Maswa) kuwa maeneo ya kibiashara.

Aidha, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi na Halmashauri ya Wilaya Maswa kutumia fursa hiyo kujenga vituo vya mabasi vya kimkakati vitakavyoendana na kasi ya uingiaji wa magari mengi baada ya kukamilika kwa barabara ya Maswa-Bariadi na Ujenzi wa Reli ya “Standard Gauge” na  Bandari kavu itakayojengwa Malampaka wilayani Maswa.

Akiwasilisha taarifa ya barabara zinazosimamiwa na TANROADS, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent amesema Barabara ya Bariadi-Maswa itajengwa kwa kutumia fedha za Serikali ya Tanzania na itachukua muda wa miezi 24 mpaka kukamilika kwake, ambapo amebainisha kuwa Mkandarasi Kampuni ya M/s CHICO ameshawasili eneo la kazi(site).

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini ameomba wazo la marekebisho ya Viwango vya fedha zinazotakiwa kwenda TANROADS na TARURA ambalo lilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, lifanyiwe kazi ili TARURA wapate fedha na kufanya kazi kwa weledi pamoja na kusaidia barabara za Halmashauri zisife.

Sagini ameongeza kuwa Halmashauri zishirikiane na TARURA kutafuta namna ya kuzifanyia matengenezo barabara za Vijiji ambazo haziko chini ya usimamizi wa wakala huo (TARURA), lakini  ni za muhimu kwa maendeleo ya wananchi hususani zinazounganisha vijiji ili kurahisisha mawasiliano kati ya kijiji na kijiji.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Simiyu,Mhandisi Peter Mosha amesema mwaka 2017/2018 Mkoa huo umeidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya kufanya matengenezo kwenye mtandao wa barabara wenye jumla ya kilomita 1780.87 , madaraja na makaravati katika Halmashauri zote sita za Mkoa kulingana na mahitaji na mpango wa bajeti wa Halmashauri husika.

Naye Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Mhe. Mashimba Ndaki amesema Wakala wa Barabara (TANROADS) unapaswa kuhakikisha barabara zote zinawekewa vivuko ili kuwasaidia wananchi kuvuka kwa usalama.

Akipongeza kazi inayofanywa na TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga ameomba TANROADS kuona namna ya kufanyia kazi kona nyingi zilizopo katika barabara ya Bariadi-Lagangabili-Kisesa pamoja na kuangalia upanuzi wa barabara mbalimbali zinazosimamiwa na Wakala huo ili zisisababishe uharibifu wa magari.

Meneja wa Wakala wa Barabara Mijiji na Vijijini(TARURA) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Peter Mosha akiwasilisha taarifa ya wakala huo(Mkoa) kwa Wajumbe wa Bodi ya Barabara katikakikao cha bodi hiyo kilichofanyika Mjini Bariadi.

Meneja wa Wakala wa Barabara hapa Nchini(TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandis Albert Kent akiwasilisha taarifa ya miradi inayosimamiwa na wakala huo Mkoani humo, katika Kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe.Dkt. Seif Shekalaghe akichangia hoja katika Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe.Mashimba Ndaki akichangia hoja katika Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika Kikao Bodi hiyo kilichofanyika leo Mjini Bariadi.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa