• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Yazindua Mkakati wa Wanafunzi Kusoma Kipindi cha Likizo ya Tahadhari ya Corona

Posted on: May 5th, 2020

Mkoa wa Simiyu umezindua mpango mkakati wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kusoma katika kipindi hiki cha likizo ya dharula ya tahadhari ya ugonjwa wa homa ya mapafu ( COVID 19) inayosababishwa na Virusi vya Corona.

Akizindua mkakati huo, Mei 04, 2020 katika Shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka amesema kuwa mkakati huo utawasaidia wanafunzi kupata masomo wakiwa nyumbani kutoka kwa walimu wao huku ukiwa na malengo makuu manne yatakayoifanya Simiyu iendelee kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.

" Malengo makuu ya mkakati huu ni kumwezesha mwanafunzi kuendelea kujifunza,walimu kuwa na mawasiliano ya kitaaluma na wanafunzi wao, wazazi kufanya ufuatiliaji wa taaluma kwa watoto wao pamoja na watoto(wanafunzi) kutulia nyumbani wakijisomea kipindi hiki cha likizo ambayo wako nyumbani, tahadhari zote za maambukizi ya Virusi vya Corona zitazingatiwa,"alisema Mtaka

Aidha, Mtaka amewataka wazazi na walezi kuwahimiza wanafunzi kutulia nyumba kujisomea na kufuatilia vipindi vya masomo mbalimbali vinavyorushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini, huku akisisitiza maelekezo yote yanayotolewa na wataalam wa afya na viongozi juu ya tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona yazingatiwe wakati wa kujisomea.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl Ernest Hinju amesema Mkoa utaendelea kufanya mawasiliano na wazazi ili siku tatu baada ya shule kufunguliwa wanafunzi wapewe mitihani ili kuwapima.

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge ametoa msaada wa kompyuta tano na printa kwa Shule ya sekondari Simiyu kutoka mamlaka ya mawasiliano kwa wote ambazo zimekabidhiwa na Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa, Christina Chenge (mke wa mbunge huyo) kwa niaba ya mbunge.

Akikabidhi kompyuta hizo, Mama Christina Chenge  amesema mbunge ametoa msaada huo na ametoa wito kuwa kompyuta hizo zitumike kwa kazi na malengo yaliyokusudiwa ili mkoa wa Simiyu uendelee kufanya vizuri katika sekta ya elimu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Mhe. Chenge kwa msaada huo na misaada mingine ambayo amekuwa akiitoa kwa shule ya Sekondari Simiyu na shule nyingine ikiwemo saruji na mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni na kusisitiza msaada huo kutumika kama ulivyokusudiwa.

Akiongea mara baada ya makabidhiano ya msaada huo, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuwa hategemei kuona shule hiyo (Simiyu sekondari) iliyokabidhiwa vifaa hivyo kupata wanafunzi wenye daraja sifuri kwani tayari wana walimu na vifaa vya kutosha sambamba na madarasa ya kutosha.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Simiyu, Paul Susu amemshukuru Mhe. Chenge kwa kutambua uhitaji walionao kwani utawasaidia katika kutekeleza shughuli zao za ufundishaji huku akiongeza kuwa pamoja na kuwa shule ya Simiyu ndio imekabidhiwa shule nyingine zitanufaika pia kwa kuwa wanafanya kazi kwa ushirikiano na shule nyingine.

Nao baadhi ya walimu wa shule hiyo akiwemo Dorine Bella na John Mogela wamesema kuwa ujio wa kompyuta hizo utakuwa chachu ya kurahisisha ufundishaji na kutekeleza mkakati wa mkoa wa wanafunzi kusoma katika kipindi hiki cha ugonjwa wa homa ya mapafu na baada ya ugonjwa huo.

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KUUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/05/simiyu-yazindua-mkakati-wa-wanafunzi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa