• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Yazindua Kampeni ya Elimu Dhidi ya Maambukizi ya Corona

Posted on: April 3rd, 2020

Mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na wadau wa afya umezindua rasmi kampeni ya kupambana na Maambukizi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona kupitia utoaji wa elimu, ambapo Shirika la Msalaba Mwekundu limeanza kutoka elimu ya tahadhari ya ugonjwa huo katika Wilaya zote mkoani hapa hususani katika maeneo yenye muingiliano wa watu wengi kama vile stendi na masoko.

Akizindua kampeni hiyo Aprili 03,2020 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amelishukuru Shirika la msalaba mwekundu kwa kujitoa kutoa elimu ya tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona na kuwataka wataalam watakaotoa elimu hii kuendelea kuwahimiza wananchi kuzingatia maelekezo ya viongozi na wataalam wa afya ikiwa ni pamoja na kuepuka kupeana mikono, kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima, matumizi sahihi ya vitakasa mikono na kuhakikisha wananawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.

“Sisi kama mkoa tunawashukuru sana Red Cross(Shirika la msalaba mwekundu) kwa kuanza kutoa elimu ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa wananchi, elimu hii ni vema ikaenda sambamba na kuwakumbusha wauzaji wa vitakasa mikono ili waweze kutengeneza vitakasa mikono kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na wauze kwa bei rafiki ya soko kwa wananchi,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amehimiza kuwa zoezi la utoaji elimu liende pamoja na kuwakumbusha wazazi na walezi kuwasimamia watoto wao kuhakikisha kuwa wanajisomea wakiwa majumbani katika kipindi hiki ambacho shule na vyuo vimefungwa ili wanafunzi hao waweze kufikia malengo yao hususani wanafunzi wa  madarasa ya mitihani.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Festo Dugange amesema Mkoa wa Simiyu umewashirikisha wadau wote wa afya katika kuiandaa jamii kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona katika utoaji wa elimu ambayo ndiyo kinga, utoaji wa mafunzo kwa watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya na utoaji wa vifaa tiba na vifaa kinga lengo likiwa ni kuufanya mkoa wa Simiyu kutopata maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwa upande wake Mratibu wa Mapambano dhidi ya Corona Mkoani Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba amesema Mkoa wa Simiyu utashirtikiana na wadau katika kuhakikisha kuwa tahadhari na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona yanafanikiwa.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Mkoa wa Simiyu,, Bw. Dismas Kiwale amesema Shirika hilo kwa kushirikianana watalam wa afya limekusudia kuwafikia wananchi hasa walio ndani zaidi(vijijini) na kupitia gari lao la matangazo wanatarajia kuzifikia kata zote na halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu ambapo watakuwa wakitoa  elimu katika maeneo yenye muingiliano wa watu wengi na kugawa vipeperushi vyenye elimu juu ya tahadhari dhidi ya Corona.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI TAFADHALI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/04/simiyu-yazindua-kampeni-ya-elimu-dhidi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa