• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu yajipanga kutengeneza Ajira kupitia Sanaa, Utamaduni na Michezo

Posted on: July 31st, 2017

 Mkoa wa Simiyu umejipanga kurasimisha kazi za sanaa, utamaduni na baadhi ya michezo ili kutengeneza ajira kwa wananchi ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu Tamasha la “Simiyu Jambo Festival” litakalohusisha mashindano ya mbio za baiskeli na ngoma za asili ambalo litafanyika Agosti 06, 2017 Mjini Bariadi.

Amesema Mkoa wake umekusudia kuandaa utaratibu wa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Sanaa Bagamoyo na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kuona namna ambayo kazi za sanaa,utamaduni na michezo zinazofanyika katika mkoa wa Simiyu zinaweza kufanywa kibiashara na zikawanufaisha wananchi.

Ameongeza kuwa vikundi vya sanaa na utamaduni vya Mkoa wa Simiyu vitapewa mafunzo ya namna ya kufanya kazi zao kitaalam katika viwango vinavyotakiwa, ili kazi ziweze kuuzika ndani na nje ya mkoa hususani kipindi ambacho watalii wengi wanakuja hapa nchini kwa kuwa mkoa huo unapakana na mikoa yenye hoteli nyingi za kitalii.

“Simiyu ni mkoa unaopakana na mikoa yenye Hoteli za kitalii, tungehitaji tufike mahali ambapo kazi za utamaduni na sanaa ndani ya mkoa wetu zinafanywa kibiashara;wakati watalii wanapotembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kwenda kwenye  hoteli za kitalii wasiishie kupiga picha, tungehitahi vikundi vyetu vya sanaa na utamaduni viuze kazi zao huko” amesema Mtaka

.Aidha, Mtaka amefafanua kuwa katika kufanikisha hayo Mkoa umeanza na mchezo wa  Mbio za baiskeli kupitia Mashindano yatakayofanyika Agosti 06, mwaka huu ambapo Mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson.

 Amesema vijana wengi wa Mkoa huo wanafanya vizuri katika mchezo huo hivyo watafanyiwa utaratibu wa kupewa mafunzo ya kuwaimarisha zaidi katika mchezo huo, ili Mkoa ufikie hatua ya kutoa wawakilishi katika nchi kwenye mashindano makubwa ya mbio za baiskeli kama ya Jumuiya ya Madola na Olimpiki.

“Tuko kwenye kutambua vipaji vya watu na tunajaribu kuona kila mwananchi aliyeko ndani ya mkoa wa Simiyu kile ambacho amejaliwa na Mwenyezi Mungu kinamsaidia kujipatia kipato chake.Tunafanya yote haya kwenye Mkoa kwa kuwa tunaamini Kipaji cha mtu ni biashara na kipaji ni ajira” amesema Mtaka.

 Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha baiskeli Mkoa wa Simiyu Joseph Paul amesema kuwa chama chake kinaiwashukuru kampuni ya Jambo Food Product kwa kudhamini mashindano hayo ya Mbio za baiskeli ambayo yatahusisha makundi matatu; kilometa 200 kwa wanaume, Kilometa 80 wanawake na Kilometa Tano kwa watu wenye Ulemavu.


Paul amesisitiza kuwa chama chake kimejipanga vilivyo na zaidi ya washiriki 150 wamethibitisha kushiriki mashindano hayo kutoka katika mikoa ya Simiyu,Geita,Mwanza, Shinyanga na Arusha

Naye Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Jambo Food  Product Anthony Paul,amesema Kampuni hiyo ambayo ni wadhamini wakuu wa Mashindano hayo wamejipanga kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo Pikipiki itakayotolewa kwa mshindi wa Kwanza (wanaume) na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 8 zitashindaniwa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)ofisini kwake kuhusu Simiyu Jambo Festival itakayohusisha mashindano ya Mbio za Baiskeli na burudani ya ngoma za asili yatakayofanyika Agosti 06 mwaka huu mjini Bariadi

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa