• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Yajipanga Kimkakati Kuongeza Kiwango cha Ufaulu kwenye Elimu

Posted on: February 14th, 2018

Mkoa wa Simiyu umejipanga kimkakati katika  kuhakikisha unaongeza ufaulu kwenye Elimu na kuwa miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri Kitaifa kutoka mahali ulipo sasa,  kwenda kwenye nafasi ya tarakimu moja(single digit) yaani nafasi ya kwanza hadi ya tisa.

Hayo yalibainishwa katika kikao maalum kilichofanyika jana Mjini Bariadi kati ya Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, kilichofanyika jana Mjini Bariadi.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewataka walimu pamoja na watendaji wengine wa idara ya Elimu kuongeza bidii katika maeneo yao ili waweze kuufikisha mkoa katika nafasi ya tarakimu moja (single digit) kwa kuwa sababu, uwezo na nia ya kufika hapo ipo.

“Watu wa Sekta ya elimu Ombi langu kwenu wakati tukiwa tunajipongeza kuwa wa 14 katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017 tudhamirie kuongeza bidii ili tuingia kwenye ‘single digit’, sababu za kuingia kwenye ‘single digit’ zipo, uwezo upo kwa kuwa ninyi mpo na nia ya Simiyu kuonekana juu tunayo” alisema Sagini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema  miongoni mwa mambo yatakayofanya mkoa huo kuendelea kufanya vizuri ni pamoja na kuendeleza makambi kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ambayo yatasaidia kuwaandaa vema na Mitihani ya Taifa.

Aidha, Mtaka amesema mkoa huo umeandaa Mpango Mkakati wa TEHAMA ambayo katika sekta ya elimu itasaidia kutekeleza mpango wa madarasa ya mitihani kusoma kwa kupitia mitandao na tayari umepokea kompyuta 60 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi  ambazo zitaweka katika shule zenye mifumo ya TEHAMA ili kuwezesha mpango huo.

Wakati huo huo Mtaka amesisitiza juu ya eneo la umuhimu wa chakula kwa wanafunzi ambapo amemuagiza Afisa Elimu Mkoa kuitisha kikao cha Wenyeviti wa Kamati za Shule, waweze kuzungumza namna ya nzuri ya kuwawezesha wanafunzi kula chakula wawapo shuleni, ili wasome vizuri baadaye waweze kufanya vizuri katika masomo yao..

“ Kama tunataka kuwa mkoa bora na kushindana kwenye elimu wazazi wakubali kuchangia chakula ili watoto wale shuleni, nitakaa na wazazi niwaambie ukweli watoe sehemu ya chakula cha nyumbani kije shuleni  na waweke utaratibu wa kuwapikia watoto ili wale shuleni; mtoto akiona moshi jikoni akili inachemka” alisema Mtaka.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory alisema uwezo wa mkoa huo  kufikia nafasi ya tarakimu moja(single digit) upo  kwa kuwa,  tangu mkoa huo ulipoanzishwa mwaka 2012 umekuwa ukifanya vizuri hususani katika Mtihani wa Kidato cha Nne, ambapo ulitoka katika nafasi ya 17, nafasi ya  14 miaka miwili mfululizo na kufikia nafasi ya 11 mwaka 2017.

Nao baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa shule walisema ili kufikia azma ya Mkoa huo kushika nafasi ya tarakimu moja yaani nafasi ya kwanza hadi ya tisa(single digit) wamejipanga katika kusimamia mipango mkakati ya shule zao, kuendeleza mazoezi ya mara kwa mara, kuongeza ushirikiano na wazazi, kufautilia ratiba na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

“Kilichonisaidia mpaka shule yangu ikawa ya pili kimkoa katika mtihani wa darasa la nne ni ushirikiano na wazazi, mitihani ya ujirani mwema, watoto kula chakula cha mchana shuleni pamoja na kuhakikisha walimu wanafuata ratiba ya masomo” alisema Joseph Kasoka Mwalimu Mkuu Shule ya msingi Halawa  wilayani Bariadi.

Kikao cha watendaji wa Idara ya Elimu kiliwahusisha Maafisa Elimu wa Wilaya, Wadhiti Ubora wa Elimu, Waratibu wa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na baadhi ya Walimu waliofanya vizuri katika masomo yao kwenye  Mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, lengo likiwa nikutambua juhudi zilizofanyika kwa mwaka 2017.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:- https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/simiyu-yajipanga-kimkakati-kuongeza.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa