• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Yaandaa Mazingira Wezeshi Kwa Wawekezaji, Yaahidi Kutoa Ardhi Ya Uwekezaji Bure

Posted on: September 13th, 2018

Serikali mkoani Simiyu imesema imeandaa mazingira wezeshi kwa wawekezaji katika Fursa  mbalimbali za uwekezaji  ikiwemo viwanda, kilimo na teknolojia, ambapo imejipanga kutoa ardhi bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga  ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo , Mhe. Anthony Mtaka katika Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Kiswaga amesema mkoa huo ni mkoa wenye ajenda ya maendeleo, hivyo umejipanga katika kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji katika fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani humo, ikiwa ni pamoja na  sekta ya viwanda, kilimo, tekonolojia mbalimbali, uchimbaji wa visima na fursa nyingine, ili kufikia lengo kuufanya mkoa huo kuwa  katika nafasi nzuri kiuchumi.

“Mkoa wa Simiyu una fursa nyingi mkifika hapa chagueni tu sehemu mje kuwekeza, mtu atakayekuja kujenga kiwanda kikubwa, kizuri ardhi tutampa bure, sisi tutamuuliza tu kwamba tuandike jina gani kwenye hati na tutamkabidhi hati yake, kwa hiyo ATAPE pelekeni salamu kwa wawekezaji wenzenu kuwa ardhi ya uwekezeaji Simiyu ni bure, ninyi mtafute mtaji tu” alisema Kiswaga.

Ameongeza kuwa wawekezaji wote watakaowekeza mkoani Simiyu watapata soko la uhakika la bidhaa zao, huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu na mikoa inayouzunguka ina wakazi wasiopungua milioni 10 ambao watakuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa zao watakazozalisha.

Aidha, Kiswaga ametoa wito kwa wawekezaji wote wakiwemo ambao ni wanachama wa  Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), kuwekeza katika ujenzi wa hoteli na hosteli katika Eneo la Nyakabindi mahali ulipo Uwanja wa Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi ili kukabiliana na changamoto ya malazi.

Katika hatua nyingine Kiswaga ametoa wito kwa Taasisi za Madhehebu ya Dini kuiga mfano wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE) katika  kuwajenga waumini wao kiroho na kuwaimarisha kiuchumi, ili Taasisi kama hizo zitumike kama madaraja kuwavusha waumini wao kueleka katika Uchumi wa Kati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), Bw. Fredy Manento amesema pamoja na kutoa huduma za kiroho ATAPE inatoa mafunzo ya  ujasiriamali,  imeweza kuwafikia zaidi ya wananchi 20,000 kupitia huduma za afya za bure na imewekeza zaidi ya shilingi milioni 639 katika miradi mbalimbali.

Makamu Mwenyekiti wa ATAPE Taifa (Upande wa Uwekezaji) Dkt. Dastan Kabiaro amesema katika uwekezaji huo ATAPE imeanza na kilimo ambapo  imeshanunua jumla ya ekari 10,250 katika mikoa ya Tanga, Iringa, Pwani , Njombe na inatarajia kupata eneo jingine katika Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kilimo cha miwa ya sukari.

“ ATAPE imeanza kuwekeza katika kilimo,baadaye tutaenda kwenye maeneo mengine ambayo tumeshaanza kama maji, tutatoa visima \Tanzania nzima kwenye  maeneo yote ambayo hayana maji; katika kilimo tumeanza kuchukua ardhi na kuiendeleza mpaka sasa tuna ekari 10,250, tumeendeleza ardhi hiyo kwa asilimia 10 na tunaendelea kuiendelea ardhi hiyo” alisema.

Mwenyekiti wa ATAPE Kanda ya Bariadi, Bi. Mariam Manyangu amesema  mkoa wa Simiyu una wanachama takribani 80, ambao miongoni mwao ni watalaam katika fani mbalimbali pamoja na wafanyabiashara na wanaendelea kuhamasisha waumini wengi kujiunga na chama hicho,  ili kujenga waumini imara kiuchumi watakaoweza  kuendesha maisha yao na kuchangia kazi ya Mungu.

ATAPE  ni kifupi cha Association Of Tanzania Adventist Proffessionals and Enterpreneurs -Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato)-ambacho kilianzishwa mwaka  1999 kwa lengo kuwafanya Wanataaluma na Wajasiriamali watumie talanta zao kwa faida ya Jamii, Kanisa na kazi ya Mungu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/09/simiyu-yaandaa-mazingira-wezeshi-kwa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa