Mkoa wa Simiyu umeahidi kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajia kufanyika Oktoba mkoani Kagera.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga Agosti 28, 2020 wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa BAKWATA wa Mikoa ya Simiyu na Kagera waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu kushiriki katika kufanikisha Maulidi hiyo.
“Tumelipokea jambo hili kwa mikono miwili na tunaahidi kulifanyia kazi kwa wepesi kwa kushirikiana na viongozi, ninaomba kupitia Katibu wa BAKWATA wa Mkoa wetu tutakaa pamoja tuone namna tutakavyolitekeleza na baadaye tutalifanyia maamuzi ndani ya muda mfupi tu ili maandalizi yaendelee,” alisema Bi. Mmbaga.
Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta amesema ili sherehe ya Maulidi Kitaifa iweze kufanikiwa inahitaji ushirikiano wa Viongozi wa mikoa jirani jambo ambalo limekuwa likifanyika wakati wote huku akisisitiza kuwa anashukuru mkoa wa Simiyu kuonesha utayari wa kushiriki kufanikisha siku hiyo.
“Tumetoka Kagera tukiwa na Baraka zote za Mhe. Mkuu wa Mkoa wetu na alituhakikishia kuwa ameshawasiliana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu hivyo tunategemea kupata ushirikiano kutoka Simiyu kwa kuwa sisi ni mikoa jirani, kama mlivyoshiriki mwaka jana kupitia kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa Mhe. Mtaka Mkoani Mwanza naamini hata mwaka huu tutakuwa pamoja ,” alisema Sheikh Kichwabuta.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/simiyu-yaahidi-kushiriki-kikamilifu.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa