• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Kupata Chupa Milioni Tatu za Viududu kwa Zao la Pamba

Posted on: March 7th, 2019

Mkurugenzi Bodi ya Pamba nchini, Bw. Marco Mtunga amesema Mkoa wa Simiyu utapokea chupa milioni tatu za viuadudu lengo likiwa kukabiliana na changamoto ya wadudu waharibifu wa zao la hilo.

Mtunga ameyasema hayo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Omari Mgumba mkoani Simiyu Machi 06, 2019 ambapo amebainisha kuwa tayari bodi imeshasambaza chupa milioni moja na laki tatu za viuadudu hivyo kwa mkoa huu na kuongeza Simiyu pekee itapokea chupa milioni tatu za viuadudu kwa msimu huu.

“Mpaka sasa chupa milioni moja zimeshafika Mwanza kwa ajili ya Mkoa wa Simiyu kila wilaya itapata chupa laki mbili, awali tulishagawa chupa milioni moja na laki tatu; kutokana na pamba iliyomwa kwa wingi Simiyu lengo letu ni kuipa Simiyu chupa milioni tatu kati ya chupa milioni nane tutakazosambaza nchini msimu huu” alisema Mtunga

Aidha, Mtunga amesema Mkoa wa Simiyu uko katika nafasi ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo la pamba kutoka kilo milioni 113 za msimu uliopita mpaka kufikia kilo zaidi ya 300 msimu huu, kutokana na pamba ilivyolimwa kitaalamu na uwepo wa idadi ya miche inayotakiwa kwa ekari.

Akiwa ziarani mkoani hapa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Omary Mgumba amesema suala la mbegu za pamba limeenda vizuri hivyo ni vema likaenda sambamba na usambazaji wa viuadudu na kuongeza kuwa wakulima wa zao hilo wameongezeka kutokana na zao hilo kufanya vizuri hususani mkoa wa Simiyu ambao umeongoza kwa uzalishaji ikilinganishwa na mikoa mingine inayolima pamba hapa nchini.

“Suala la mbegu lilienda vizuri lakini kubwa zaidi ni mahitaji makubwa kuliko matarajio kutokana na hamasa mliyofanya mwaka jana watu wengi walihamasika kulima pamba, hata mwaka huu wengi zaidi watakuwa wamelima, maana wakulima wengi huwa wanahamasika kulima zao ambalo limefanya vizuri msimu uliopita” alisema Mgumba.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa lengo la mkoa ni kuongeza uzalishaji kwa ekari kuanzia kilo 500 hadi 1000 kwa ekari badala ya kuongeza idadi ya wakulima pekee.

“Tungehitaji kuongeza uzalishaji kwa ekari badala ya kuongeza uzalishaji kwenye idadi ya wakulima, mwaka 2018 tulivuna kilo milioni 113, mwaka huu uzalishaji utaongeza lakini unaweza kuongezeka kutokana na ongezeko la wakulima na ekari zilizolimwa; wakati tunaweza kupata kilo kama hizo kwenye pungufu ya ekari na idadi ya wakulima kama tutaongeza uzalishaji kwa ekari”

“Msukumo wa Mkoa ni kuona tunaongeza uzalishaji kwa ekari, ukienda Mwabusalu kuna wakulima wanazalisha kuanzia kilo 500 hadi 1000 kwa ekari , kwa hiyo kama mkoa tumejipanga kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kwa ekari na idadi ya wakulima pia inaongeza” alisema Mtaka.

Naibu Mgumba yuko mkoani Simiyu katika ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua shughuli za kilimo na ushirika zinavyoendelea pamoja, kukagua shughuli za miradi ya umwagiliaji akiwa Wilayani Itilima amepata nafasi ya kuzugumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KATIKA HABARI HII FUNGUA KIUNGANSHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/03/simiyu-kupata-chupa-milioni-tatu-za-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa