Bariadi,
Jumla ya Shule 8 za Msingi Mkoani Simiyu zimenufaika na vifaa mbalimbali vya TEHAMA vilivyotolewa na Serikali kupitia Mradi wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anna Joram Gidarya amekabidhi vifaa hivyo leo 19 Aprili 2024 kwa wakuu wa shule za Msingi 8 zilizopata mgao wa vifaa hivyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
“Rai yangu kwenu ninyi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda,nendeni mkafanye kazi.Hii inaaonyesha ni jinsi gani Mhe.Rais anawathamini ninyi walimu”.Alisema Mhe.Gidarya.
Awali akizugumza na Maafisa Elimu pamoja na wakuu wa shule waliofika kwa ajili ya kukabidhiwa vifaa hivyo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo ametoa rai kwa Walimu waliopokea vifaa hivyo kuvitunza pamoja na kuvitumia kwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akisoma taarifa ya mapokezi ya Vifaa hivyo kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu Bw.Erasmus Buretta amesema Mkoa wa Simiyu kwa awamu ya kwanza ulipokea jumla ya Kopyuta za mezani 40,Printa 8 na UPS 24 na kusambazwa katika vituo 8 ambapo kwa awamu ya pili Mkoa umepokea jumla ya Kompyuta mpakato 16,Mashine za Photocopy 8,Projecta 16,Skrini na Stendi 16,Smart TV za Nchi 65,Microphone 8,Zoom Camera 8,Digital Camera 8, na Wireless router 8.
Ameeleza kuwa tayari Walimu 16 na Maafisa TEHAMA 6 wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia vifaa hivyo yaliyofanyika Jijini Mwanza katika Chuo cha Ualimu Butimba Mwezi Februari 2024.
Kwa upande wao walimu pamoja na Maafisa Elimu walionufaika na Vifaa hivyo,wameishukuru Serikali kwa uwezeshaji huo ambapo wameahidi kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Shule zilizonufaika na vifaa hivyo ni pamoja na Shule ya Msingi Nyakabindi,Ngulyati,Nyashimo,Luguru,Binza,Malampaka,Mwanhuzi pamoja na Mwabuma.
GCO,
Simiyu RS
19 Aprili 2024.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa