• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Yawafichua Watoto 16,000 Wenye Ulemavu Waliofichwa na Kuwaandikisha Shule

Posted on: December 3rd, 2019

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa amesema Serikali imewafichua na kuwatambua jumla ya watoto 16,000 wenye ulemavu wa aina mbalimbali waliokuwa na umri wa kwenda shule katika mikoa yote hapa nchini waliokuwa wamefichwa na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi.

Naibu waziri Ikupa ameyasema hayo Desemba 03, 2019 katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

“Watoto wenye mahitaji maalum waliokuwa wamefichwa Serikali imewatambua na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi, watoto 16,000 wametambuliwa kutoka mikoa na halmashauri zote nchini isipokuwa Halmashauri tisa tu ambazo hazijafikiwa kwa kuwa zoezi hili ni endelevu kadri bajeti itakavyoruhusu nazo zitafikiwa,”alisema Ikupa.

Aidha akijibu baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na  Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) kuhusiana na kutengewa bajeti ndogo amesema kuwa tayari serikali imetenga milioni 30 kwa ajili ya kuliwezesha baraza la watu wenye ulemavu kufanya kazi kwa ufanisi, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuongeza nguvu katika kuwasaida watu wenye ulemavu hususani walio katika maeneo ya pembezoni.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ikupa ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutenga nafasi maalum za uwakilishi bungeni kwa watu wenye ulemavu kama kilivyofanya Chama Cha Mapinduzi( CCM), huku akiwasisitiza wenye ulemavu na wao kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kusubiri nafasi maalum pekee.

Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesema Simiyu inawathamini na kuwajali watu wenye ulemavu huku akibainisha kuwa Halmashauri zimetenga zaidi ya shilingi milioni 231 katika mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa watu wenye ulemavu na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo ili wajikwamue kiuchumi.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Bibi. Tungi Mwanjala ameiomba Serikali kuviwezesha viwanda vya ndani kutengeneza vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ili kupunguza gharama zitokanazo na kodi ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Naye mmoja wa Watu wenye ulemavu Bi Nuru Awadh amesema katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano watu wenye ulemavu wameaminiwa  katika nafasi mbalimbali na sheria nyingi zinazowahusu watu wenye ulemavu zitakelezwa kwa vitendo.

Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema: “HAMASISHA USHIRIKI WA WATU WENYE UELMAVU NA UONGOZI WAO: TEKELEZA AGENDA ENDELEVU 2030”

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI:- https://simiyuregion.blogspot.com/2019/12/serikali-yawafichua-watoto-16000-wenye.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa