• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali Mkoani Simiyu Yaitaka Jamii Kushiriki Kikamilifu Kupinga Mimba za Utotoni

Posted on: June 16th, 2018

Serikali Mkoani Simiyu imeitaka jamii kushiriki kikamilifu katika suala la kupinga mimba za utotoni ili kukabiliana na ongezeko la mimba lililofikia 195 kwa wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari katika kipindi cha miaka mitatu  mkoani humo.

 Wito  huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.  Benson Kilangi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika, yaliyofanyika Kimkoa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nanga B wilayani humo na kuhudhuriwa na wananchi na wadau wa maendeleo lengo likiwa ni kuikumbusha jamii haki za Mtoto.

Kilangi amesema Serikali haitawafumbia macho wale wote watakaowapa mimba wanafunzi hivyo akawataka wananchi kuungana na Serikali katika kulaani na kufichua wale wote wanaojihusisha na suala hilo ambalo linasababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao.

“ Mpaka kufikia  mwaka 2016/2017 watoto 195 kati yao 25  wa shule za msingi na sekondari 170 wamepata mimba ndani ya mkoa wetu, hili ni tatizo na sisi hatutamfumbia macho wala kumlea mtu yeyote atakayempa mimba mtoto wa shule, niwaombe wananchi wote muungane na Serikali kulaani kwa nguvu zote mimba kwa watoto wetu wa kike” alisisitiza Kilangi

Katika hatua nyingine Kilangi amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoani Simiyu kuunda mabaraza ya watoto ambayo yatalenga kusaidia katika kuwapatia watoto fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo stadi za maisha zitakazowafanya wawezekutambua haki zao, kujieleza na kupata mbinu za kukabiliana na  changamoto wanazokutana nazo katika jamii

Baadhi ya wanafunzi wameiomba Serikali kuwachukulia hatua kali wale wote wanaowarubuni wanafunzi wa kike na kuwapa mimba hali inayochangia wanafuzi hao kukosa haki ya msingi ya kupata elimu na kufikia kwenye ndoto zao.

“Watu wanaowapa mimba wanafunzi wapewe hukumu kali maana wanachangia wanafunzi kuacha shule halafu wanashindwa kufikia malengo yao, kwa mfano waliokuwa  na mpango wa kuendelea na elimu ya juu wanaishia njiani sababu ya mimba, mimi naona serikali iwafunge tu” Kabula Masanja mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nanga B.

“Wapo wanafunzi wa kike wamepata mimba kutokana na vishawishi vya baadhi ya watu wasio waaminifu na Serikali imeanza kuchukua hatua kwa wote waliobainika kuhusika na kosa hilo, tunaomba Serikali iendelee kuwachukulia hatua ili tabia hii ikomeshwe kabisa na wanafunzi wa kike wabaki salama “ alisema Luhangija Maduhu mwnafunzi Shule ya msingi Nanga akisoma risala ya watoto wa Mkoa wa Simiyu

Naye Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la World Vision, Ngasa Michael  amesema shirika hilo linaungana na Serikali katika vita dhidi ya mimba za utotoni ambapo wamekuwa wakishirikiana na  viongozi wa dini na Serikali katika jamii hususani  katika maeneo yote ambayo shirika hilo linafanya kazi mkoani Simiyu , huku akibainisha kuwa sasa jamii imeanza kuelewa athari za mimba za utotoni kwa watoto wa kike katika kiafya, kielimu na kijamii


Katika maadhimisho hayo ya Mtoto wa Afrika ya Mwaka 2018 ambayo Kauli Mbinu yake ni “Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tusiwaache Watoto Nyuma” Shirika la World Vision limekabidhi madaftari,kalamu na vifaa vya Michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa wanafunzi shule 15 Wilayani Itilima.

MWISHO 



Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa