Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Mkoani Simiyu unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 51 ya mwaka 2019 hadi 57.4 ifikapo 0ktoba 2020 kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo (P4R ) hali itakayosaidia wananchi kuepukana na adha ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa uhakika na urahisi.
Hayo yamesemwa Septemba 11, 2020 na meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) mhandisi Mariam Majala wakati wa makabidhiano ya mabomba yatakayotumika kutekeleza miradi ya maji Mkoani Simiyu yaliyofanyika katika ofisi za RUWASA mjini Bariadi.
“Tayari tumepokea mabomba asilimia 70 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo yana thamni ya zaidi ya shilingi milioni 800, tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa mradi wa P4R na tunaamini tutakapokuwa tumelaza mabomba haya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii na tutakuwa tumeongeza maji kwa asilimia 6.4, kutoka asilimia 51 hadi 57.4,” alisema Mhandisi Manjala.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewapongeza watendaji wa RUWASA Mkoa wa Simiyu kwa namna wanavyotekeleza miradi kwa kasi huku akibainisha kuwa mradi wa P4R utatoa ajira kupitia utandazaji wa mabomba hivyo akatoa wito kwa Wana Simiyu kuchangamkia fursa hiyo ya ajira pamoja
Aidha, Mmbaga ametoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu hiyo ya maji itakayotandazwa katika maeneo hayo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa P4R ili kuweza kuusaidia mkoa kufikia azma ya kuongeza hali ya upatikanaji wa maji.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Zabuni ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyotumika kuandaa mchakato wa manunuzi wa mabomba hayo, Bw. Ekwabi Mujungu amesema anawapongeza RUWASA kwa kununua mabomba kulinga na sifa zilizoandishwa na kupitishwa na bodi hiyo huku akisisitiza miradi kwenda kutekelezwa kwa kiwango bora ili thamani ya fedha.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/09/ruwasa-simiyu-yaahidi-kuongeza-hali-ya.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa