• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

Posted on: December 17th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesitisha matumizi ya leseni 18 za uchimbaji madini katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa wilaya ya Bariadi na Busega, mpaka pale zitakapotolewa ufafanuzi na Waziri mwenye dhamana ya madini juu ya uhalali wake katika uendeshaji wa shughuli za madini.

Mtaka ametoa uamuzi huo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika eneo la mgodi Desemba 17, 2020 akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kwa ajili ya kwenda kusikiliza kero za wachimbaji wadogo mgodini hapo na kuzitafutia ufumbuzi.

“Sisi kama viongozi wa mkoa tunasitisha matumizi ya leseni za eneo lote hili, mpaka pale waziri mwenye dhamana atakapokuja kutoa ufafanuzi kwa wananchi, kwa sababu sheria inamtamka waziri kwenye kufuta leseni lakini sisi mkoa kwa tuliyoyaona hapa tunasitisha; kwa sasa  mgodi utaendelea kuwa chini ya usimamizi wa maelekezo ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema Maafisa kutoka katika Ofisi zote zinazopaswa kutoa huduma kwa wachimbaji hao ikiwa ni pamoja na maafisa wa Soko la Madini kuanzia Desemba 18, 2020 watakuwa katika eneo la mgodi ili kuwapunguzia wachimbaji hao adha ya kufuata huduma mbali na eneo hilo huku akisisitiza wachimbaji hao wauze dhahabu kwa bei iliyopo sokoni.

Mtaka pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Bariadi na Busega kufanya tathmini ya mashamba yaliyoharibiwa na shughuli zinazoendelea katika eneo la mgodi ili wakulima hao waweze kulipwa fidia, huku akiwataka Wakurugenzi hao  pia kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa matundu ya vyoo yasiyopungua 12 kuimarisha hali ya usafi mgodini.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa onyo kwa wachimbaji na watu wote wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji madini kujiepusha na utoroshaji wa dhahabu, kwamba  watakapobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutaifisha dhahabu hiyo.

Awali wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba na wamiliki wa maduara  waliwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye mgodi huo ambazo baadhi zilipatiwa ufumbuzi  na uongozi wa mkoa na baadhi zitashughulikiwa na Waziri mwenye dhamana ya madini.

“Usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwenye mgodi huu uimarishwe zaidi, ili Serikali ipate sehemu yake, wachimbaji na sisi tupate sehemu yetu na kila tozo au ushuru wanaotutoza wahakikishe wanatoa risiti za kielektriniki,” alisema Flugence Ekondo mchimbaji mdogo.

“Katika ugunduzi wa mgodi huu mke wangu alikuwa anapalilia mahindi akaokota jiwe, alivyolileta tulikuwa na wasiwasi nalo tukalipeleka mgodi wa Gasuma tukaambiwa ni dhahabu, hiyo ilikuwa tarehe 05/11/2020 kesho yake wachimbaji wakaanza kuchimba na mgao ukafanyika; binafsi nilijua hiyo itakuwa rashi itakayotunufaisha wachimbaji wadogo na jamii inayotuzunguka,lakini baadaye tukasikia kuna leseni tunaomba tusaidiwe na sisi tupate haki yetu kwenye mgao,” Ntimba Masalu mwakilishi wa wenye mashamba

Akitoa ufafanuzi kuhusu mgao, Afisa madini Mkazi wa Mkoa, Mhandisi. Oscar Kalowa amesema “katika mifuko 100 asilimia saba ni fedha ya serikali, wamiliki wa mashamba asilimia 15, msimamizi/mmiliki wa leseni asilimia 15 na mwenye duara husika anapata asilimia zinazobaki na huu ndiyo utaratibu unaohusika.”

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/12/rc-simiyu-asitisha-leseni-za-uchimbaji.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa