RC NAWANDA ARIDHISHWA NA UJENZI MRADI WA MAJI MWABUMA/MWASHATA MEATU.
Meatu,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda ameridhishwa na maendeleo ya Ujenzi wa mradi wa Maji wa MWabuma/Mwashata unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 900.
Zaidi ya Wananchi 6000 wanatarajia kunufaika na mradi huo utakapokamilika Mwezi Julai 2024 ambapo hadi kufikia Tarehe ya Leo utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo umefikia Asilimia 40.
Dkt.Nawanda ameshauri kuzingatiwa ujenzi wa miundombinu ya kunyweshea mifugo katika Miradi ya Maji inayotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA ili kutoa fursa kwa wafugaji kunufaika pia na miradi hiyo.
Amesisitiza Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kukamilika kwa wakati ndani muda uliopangwa pamoja na kuzingatiwa ubora na viwango.
Ametoa wito kwa Wananchi kutumia fursa ya mradi huo kusogeza huduma ya Maji majumbani mwao ili kuepuka adha ya kufuata umbali mrefu.
GCO,
Simiyu -RS
30 Mei 2024
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa