• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RC Mtaka: Kambi za Kitaaluma Simiyu Zitakuwa Endelevu

Posted on: April 28th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Kambi za Kitaaluma mkoani Simiyu kwa wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha Sita, ambayo ni madarasa yanayofanya Mitihani ya Taifa ya kuhitimu elimu ya Msingi na Sekondari zitakuwa endelevu.

Mtaka amesema hayo Aprili 28, 2019 wakati akihitimisha Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, iliyohusisha wanafunzi 1166 kutoka katika shule 12 mkoani hapa.

Amesema Mkoa utaendelea kufanya jitihada na kuboresha zaidi kambi hizo huku akieleza kuwa ameshawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya motisha kwa walimu na wanafunzi watakaokuwa wakifanya vizuri.

“Kambi za kitaaluma  zitaendelea kuwepo katika kipindi chote nitakacho kuwepo na tutaendelea kuboresha; mwaka huu nimewaambia Wakurugenzi ni lazima kila Halmashauri itenge fedha kwa ajili ya motisha katika elimu, motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka amewashukuru walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali waliochangia kufanikisha kambi ya kidato cha sita, huku akiwasisitiza wanafunzi wa hao kuendeleza juhudi walizozionesha wakiwa kambini na kutumia mbinu walizopewa na walimu mahiri ili waweze kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato kutoka Jijini Mwanza, Nicodemo Ntabindi amewaonya wanafunzi wa Kidato cha sita kutojihusisha na masuala ya mapenzi badala yake wajikite katika masomo tu kwa sasa ili waweze kufikia ndoto zao.

Kwa upande wao wanafunzi waliokuwepo katika kambi hiyo ya Kitaaluma wamesema kambi hiyo imekuwa msaada kwa wanafunzi kwa kuwa imechangia kuwasaidia kupata ufumbuzi wa mada ngumu zilizokuwa zinawapa shida na kuahidi kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa kutokana na namna walivyoandaliwa vema.

“Tunashukuru uwepo wa kambi hii maana imetusaidia kupata maarifa ya namna ya kujibu maswali kwenye mitihani, lakini tumeweza kusaidiwa na walimu kutatua mada ngumu ambazo zilikuwa zinatushinda, ninaamini kwa namna tulivyoandaliwa hatutamuangusha Mkuu wetu wa Mkoa” alisema mwanafunzi Farida Omary.

“Kambi hizi hazijafanyika popote hapa nchini tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kuja na wazo la kuwa na kambi kwa sababu tumejifunza mengi, tumekutana na wenzetu wa shule mbalimbali hapa mkoani kwetu na tukapata maarifa ambayo awali hatukuwa nayo, tuna imani tufanya vizuri “ alisema mwanafunzi Casto Nyakarungu.

Katika kambi hii Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, imetoa shilingi milioni 12 kwa ajili ya motisha kwa walimu waliokuwa wakifundisha kambini hapo na imeahidi kutoa shilingi milioni nne kwa mwanafunzi atakayepata ‘division one, pointi tatu’ na kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/04/rc-mtaka-kambi-za-kitaaluma-simiyu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa